SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, November 29, 2012

PRECISION AIR INAWAPA NAFASI MASHABIKI WAKE KATIKA UKURASA WA FACEBOOK KUWA WA KWANZA KURUKA NA NDEGE YAO MPYA BUURE!!‏

Baada ya shirika la ndege la Precision Air kununua ndege yao mpya aina ya ATR 42-600 na kuwa shirika la kwanza Africa na duniani kumiliki na kutumia ndege aina hiyo, sasa inawapa fursa mashabiki wake katika mtandao wa facebook na twitter kuwa wa kwanza kuruka na ndege hiyo.  Ndege hiyo hiyo ya kisasa ambayo uzinduzi wake rasmi umepangwa kufanywa tarehe 5 ya mwezi December, ina siti 50 na inatarajiwa kufanya safari zake kati ya Dar es salaam na Kilimanjaro.
Katika uzinduzi huo Precision Air itatoa zawadi kwa washindi watatu (3) kutoka katika ukurasa wao wa facebook. Ili kushinda itakubidi utembelee ukura wao wa facebook (www.facebook.com/Precisionairtz), kwanza bonyeza LIKE kama bado hujajiunga na ukurasa huo halafu SHARE picha ya ndege hiyo iliowekwa kwenye ukurasa huo kisha waambie marafiki zako waLIKE na kuCOMMENT kwenye picha yako ulioSHARE, Watu watatu (3) watakaoongoza kwa kua na LIKEs na COMMENTs nyingi kwenye picha yao walioShare moja kwa moja kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Precision Air watakua washindi.
Hi ndio picha ya shindano unayotakiwa kuSHARE ili kushinde
[ ANGALIZO : Unatakiwa kushare picha moja kwa moja kutoka kwenye facebook page ya Precision Air]

Mshindi wa kwanza kwa kua na LIKEs na COMMENTs nyingi zaidi atashinda tiket ya buuure kwenda kokote ambako ndege za Precision Air zinakwenda, pia atapata fursa ya kuruka na ndege mpya ATR 42-600  na mwisho atahudhuria sherehe za uzinduzi wa ndege hi mpya.

Mshindi wa pili atapata fursa ya kuruka na ndege mpya ATR 42-600  na pia atahudhuria sherehe za uzinduzi wa ndege hi mpya. Na mshindi wa tatu yeye atapata fursa ya kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa ndege hi mpya.

Kwa maelezo zaidi tembelea kurasa zao za; facebook [www.facebook.com/precisionairTz],

0 comments:

Post a Comment