Sharo Milionea
Kwa mujibu wa wananchi wa eneo ilikotokea ajali hiyo, walishindwa kumchukua msanii huyo angalau kumkimbiza hospitalini kutokana na kijiji hicho kukosa mtu anayemiliki gari, pikipiki wala baiskeli na walipopiga simu Polisi, askari walifika hapo saa 4 usiku na kuuchukua mwili.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa msanii huyo alikuwa akienda nyumbani kwao kusalimia wazazi wanaoishi Lusanga akitumia gari hilo.
“Ajali hii ilitokea baada ya dereva kushindwa kumudu gari hilo kwa kuwa lilikuwa na mwendo mkali, kwa hiyo alipofika hapo liliserereka na kuacha njia na kuingia kwenye mtaro pembeni mwa njia,” alisema mkazi wa Maguzoni aliyejitambulisha kwa jina la Saidi.
Wengine walidai kuwa msanii huyo alirushwa nje ya gari baada ya ajali hiyo, kwani hata walipofika eneo la tukio walimkuta akiwa nje ya gari hilo. Walipochunguza zaidi ndani walishuhudia mifuko ya hewa imefunguka, hali inayoashiria pengine hakuwa amefunga mkanda.
Akithibitisha hilo, mtangazaji wa kituo cha redio na televisheni cha Clouds Media, Millard Ayo, aliyefika eneo hilo, alisema Sharo Milionea alikutwa nje ya gari na watu waliofika hapo mara baada ya ajali kutokea, lakini hakuwa amekata roho na hakuweza kuzungumza chochote.
“Walichungulia ndani ya gari ambalo lilikuwa limeharibika sana hawakumwona, lakini kwa pembeni nje ndiko alikuwa amelala na kwa mujibu wao, aligeuza kichwa upande wa pili na kisha kuchezesha mguu mmoja na kukata roho,” alisema Ayo.
Diwani wa Mbaramo wilayani Muheza, Seif Makame alisema alipopata taarifa za tukio, alikwenda hospitali teule kuthibitisha, lakini hakumtambua haraka kutokana na kupasuka kichwani, ingawa baadaye alithibitisha kwa kitambulisho chake kwa msaada wa maofisa wa Polisi.
Mwili wa msanii huyo unatarajiwa kuzikwa leo Lusanga. Wasanii wengine wakubwa waliopoteza maisha mwaka huu ni Steven Kanumba, Fundi Said ‘Mzee Kipara’, Khalid Mohamed ‘Mlopelo’ na Maganga.
Chanzo: dewjiblog
Kwa habari na picha ya tukio zima huko Tanga
BOFYA

0 comments:
Post a Comment