Muungano wa upinzani nchini Burundi umetangaza kumtambua rasmi Rais Pierre Nkurunziza aliyechaguliwa tena hivi karibuni na kutaka kufanya mazungumzo na serikali yake. Taarifa iliyotolewa na muungano wa vyama kumi na mbili unaojulikana kwa jina la Democratic Alliance For Change (ADC) imesema kuwa, kuna haja ya kufanyika mazungumzo baina yao na serikali kwa ajili ya kuimarisha demokrasia katika nchi hiyo. Leonce Ngendakumana, Msemaji wa Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Burundi amesisitiza kuwa, mazungumzo hayo yana nafasi muhimu kwa ajili ya amani, kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa na kuandaa mazingira ya kurejea nchini humo viongozi wa upinzani wanaoishi uhamishoni. Itakumbukwa kuwa, vyama hivyo vilisusia uchaguzi wa Rais na ule wa Bunge vikisema kuwa, hakukuwa na mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na wa haki. Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi aliapishwa siku ya Ijumaa na kukabidhiwa jukumu la kuiongoza Burundi kwa kipindi cha pili cha miaka mitano. Rais huyu alijipatia ushindi wa asilimia 91 ya kura katika uchaguzi wa Rais uliofanyika wiki chache zilizopita.
Friday, September 3, 2010
Wapinzani Burundi wamtambua Nkurunziza, wataka mazungumzo
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, September 03, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment