Mamilioni ya Waislamu katika pembe mbalimbali ulimwenguni leo watajitokeza katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambapo sambamba na kuonyesha chuki zao dhidi ya Wazayuni maghasibu watatangaza kwa mara nyingine tena uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina. Kwa mara nyingine Waislamu wanatarajiwa kuitikia wito wa Imam Khomeini MA kwa kuadhimisha na kuandamana katika Ijumaa hii ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Quds. Wananchi wa Iran pia ambao daima wamekuwa mstari wa mbele katika kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Quds. Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu ina unyeti maalumu hasa kutokana na kushadidi njama za Wazayuni na waitifaki wao dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina sambamba na kuanza mazungumzo eti ya amani baina ya Israel na Mamlaka ya Ndani ya Palestina huko Washington Marekani. Itakumbukwa kuwa, Imam Khomeini Muasisi wa Jamhuri ya Kiisloamu ya Iran aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kila mwaka kuwa Siku ya Kimatifa ya Quds na siku ya kutangaza uungaji mkono kwa wananchi madhulumu wa Palestina.
0 comments:
Post a Comment