Waasi 11 wakiwemo raia wa kigeni wamepoteza maisha nchini Somalia baada ya mabomu waliyokuwa wakijaribu kutega kulipuka mjini Mogadishu.
Duru zinaarifu kuwa wanamgambo hao walipoteza maisha katika matukio mawili tofauti, 10 walipoteza maisha wakitega bomu ndani ya gari na mwingine wakati alipokuwa akitenga bomu kando ya barabara. Wizara ya Habari ya Somalia imewataja magaidi waliopoteza maisha kuwa Wapakistani watatu, Wahindi wawili, Muafghani, Mualgeria , Wasomali wawili pamoja na kiongozi wao. Polisi wamewatia nguvuni watu wawili waliokuwa wakimlinda gaidi aliyekuwa akichimba shimo la kutega bomu katika daraja moja mjini Mogadishu na kunasa mfuko uliokuwa umejaa mada za milipuko.
Waasi wa kundi la Al Shabaab wanadhibiti maeneo makubwa ya Mogadishu katika nchi hiyo ambayo haijaweza kuwa na serikali imara katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment