SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, August 22, 2010


Futari Ya Leeds Swahili Community

Asalaam Aleykum,
Wadau wote wa globo hii.
Tunamshukuru Allah kutujaalia sote kufikia kumi hili la pili la mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, na hivyo tunawaombea baraka, afya na amani wadau wote wa globo hii waliojaaliwa kufunga Ramadhani na ambao hawakujaaliwa. Kaka michuzi, sisi Leeds Swahili Community tunawashukuru sana watu wote waliohudhulia muhadhara wetu wa leo uliofanyika katika ukumbiwa Mabegate Mill na kisha kufuturu kwa pamoja kwenye ukumbi wa Ebbo Garden

Shukurani za Pekee zimuendee Muhadhiri ; SALUM KHATIBU na wenzie kutoka London
Kwa wengine ambao hamkupata nafasi ya kushiriki nasi kwa safari hii, tunahakika Inshaalah tutashirikiana nanyi safari ijayo. Hata hivyo kwa upendo wenu tumeona tushiriane nanyi kwa kuwaonyesha baadhi ya matukio kama ifuatavyo:

Pichani juu ni Ustaadh Malick (mwenye koti) akifungua muhadhara na kumkimkaribisha rasmi muhadhiri Ustaadh Salum Khatib na pembeni kushoto mwenye miwani ni mwenyekiti Amran Rashid

Baadhi ya wahadhiriwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini
maada ya Familia na Tabia Bora (wazazi na watoto)

Wahadhiriwa wakifuatilia muhadhara

Watoto kwa wakubwa wakifuatilia mawaidha

Futari imeshaandaliwa...

wadau wakifutari

Futari ikiendelea

Leeds Swahili Community inawatakia Ramadhani
Mubaraka na Inshaallah Allah atupokelee Swaumu zetu


Asalaaam Aleykum

Wabilah Tawfiq
Mwenyekiti Amran Rashid,
Mjumbe Ustaadh Malick

0 comments:

Post a Comment