Sifa za kipekee za kiteknolojia za Kituo cha Nyuklia cha Bushehr
Mkurugenzi wa Shirika la Ujenzi na Uzinduzi wa Vituo vya Nyuklia vya Iran amesema kituo cha Nyuklia cha Bushehr kina sifa za kipekee duniani. Mohammad Ahmadian amesema kujumuishwa teknolojia za Magharibi na Russia ni sifa ya kipekee ya kituo cha Busher kilicho kusini mwa Iran katika Ghuba ya Uajemi. Ameongeza kuwa Iran itajenga vituo vya nyuklia vyenye kuzalisha megawati 25 elfu katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
Kiwanda cha kwanza cha kuzalisha nishati ya nyuklia cha Iran katika mji wa Bushehr kilianza kuwekwa fueli ya nyuklia jana. Hafla ya kuwekwa fueli katika kituo hicho imehudhuriwa na Ali Akbar Salehi Mkuu wa Taasisi ya Atomiki ya Iran na Sergei Kiriyenko Mkuu wa Taasisi ya Nyuklia ya Russia. Wakati huo huo Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA umetoa taarifa na kuthibitisha kuanza kuwekwa fueli katika kituo cha nishati ya nyuklia cha Busher. Wakala huo wa Umoja wa Mataifa wa Nishati ya Atomiki umesema utafanya ukaguzi wa kawaida katika kituo hicho cha nyuklia cha Iran.
0 comments:
Post a Comment