Waziri Mkuu wa Kenya alazwa hospitalini
Hadi sasa Raila Odinga mwenye
umri wa miaka 65 amekuwa ni mtu mwenye nguvu.
Katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigia
debe katiba mpya inayopendekezwa na hajaripotiwa kuwa na matatizo ya
kimwili.
Kwa hiyo taarifa iliyotolewa hii leo na msemaji
wake imewashangaza wengi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo madaktari wameamuru
Odinga alazwe hospitalini kwa muda wakisema tu kwamba ana uchovu. Cha
kukanganya ni kwamba taarifa hiyo iliwanukuu madaktari hao pia wakisema
Odinga ana uwezo wa kufanya kazi kama kawaida ikiwa atajisikia kufanya
hivyo. Japo hawatamruhusu kufanya hivyo.
Hadi sasa, maswali mengi kuhusu afya ya
kiongozi nchini Kenya yameelekezwa kwa Rais Mwai kibaki ambaye baada ya
uchaguzi wa mwaka 2003 kulikuwa na tetesi kwamba alipata kiarusi.
Hata hivyo maafisa wake walikanusha madai hayo
wakisema alikuwa na matatizo madogo tu ya kiafya.
******************************
Utafiti wa kimataifa umebaini kuwa Luanda,mji mkuu wa Aangola ndiyo mji wenye gharama ya juu kwa wataalamu wanaotoka nje na kwenda kufanya kazi huko.
Ripoti iliyonadiwa na kampuni ya masuala ya
kifedha ya - Mecer imesema gharama za kupanga nyumba mjini Luanda ni
mara dufu ikilinganishwa na jiji la London.
Mji wa Luanda umetajwa kuwa ghali zaidi,
ukifuatwa na Tokyo, Ndjamena na Moscow. Bara Afrika lina miji mitatu
miongoni mwa miji kumi ambayo ni ghali duniani.
Jiji la Libreville, Gabon likishikilia nafasi ya
saba. Uchunguzi ulifanyiwa katika miji 214 katika mabaraza yote
matano. Mambo yaliyoangaziwa ni pamoja na gharama za maisha ikiwemo
usafiri, chakula, mavazi na starehe.
Tiketi moja ya kutazama filamu mjini Luanda
inauzwa dola 13.
Licha ya raia wengi wa Angola na Gabon kuishi
katika lindi la umasikini, hali ni tofauti kwa wageni ambapo gharama za
maisha miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni za mafuta zinaambatana na
usalama wao pamoja na ada ya kuagiza bidhaa kutoka nchi zao.
Gharama za juu zimawalazimu wenyeji wengi
kuondoka mijini kwani hawawezi kukimu maisha.
0 comments:
Post a Comment