Milipuko Burundi wakati wa kuhesabiwa kura za
urais
Hali ya wasiwasi imetanda mjini
Bujumbura,Burundi baada ya mabomu ya guruneti kulipuka katika eneo moja
lenye watu wengi jana usiku.
Hakuna aliyekufa kwenye tukio hilo lililotokea
wakati shughuli ya kuhesabu kura za urais inaendelea katika sehemu
zengine nchini humo.
Kumekuwa na matukio ya mashambulio ya maguruneti
katika siku za hivi karibuni.
Wakati huo huo vyama vya upinzani nchini Burundi
vimesema kwamba havitatambua matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu wa
jana ambapo rais Pierre Nkurunziza alikuwa mgombea wa pekee.
Wapinzani wa rais Nkurunziza walijiondoa mchuano
wa urais wakidai udanganyifu kwenye uchaguzi wa mabaraza.
Muungano wa vyama 12 vya upinzani umesema ni
asili mia 30 pekee ya wapiga kura waliojitokeza kwenye zoezi la jana na
kuapongeza raia waliosusia uchaguzi huo.
Uchaguzi wa jana ndiyo wa kwanza tangu kundi la
mwisho la waasi kujiunga na mpango wa amani na kuitikia kushiriki katika
mchakato wa kisiasa.
Watu 10 Wakamatwa Marekani kwa kuipelelezea Urusi
Watu kumi wamekamatwa nchini
Marekani kwa kushukiwa kuwa majasusi wa Urusi.Watu hao walikamatwa
kwenye msako uliofanyika katika miji ya NewYork, Boston, New Jersey na
Virginia. Mshukiwa mwingine angali anasakwa.
Idara ya Sheria ya Marekani imetoa stakabadhi
kudhibitisha kuwa watu iliowazuilia wamekuwa wakikusanya habari za
kijasusi a kuzipokeza kwa serikali ya Urusi.
Idara hiyo inasema baada ya uchunguzi wa muda
mrefu imewanasa watu hao wakiwemo wanaume wanne na wake zao ambao
wamekuwa wakifanya kazi kichichini ili kupata habari muhimu kutoka kwa
ofisi za serikali na idara zingine muhimu.
Maafisa hao wa marekani pia wanasema washukiwa
hao wamekuwa wakiwasajili watu wengine kwa kazi hiyo ya kijasusi. Mmoja
wao anadai kuwa alikuwa ametumwa kuchunguza hasa jinsi serikali ya Rais
Obama inavyoiona Urusi kabla ya rais huyo wa Marekani kuzuru urusi.
Habari hizi zimeitia serikali ya Marekani
wasiwasi hasa kwa sababu rais Obama amekuwa akijaribu kuoberesha
uhusiano wa serikali hiyo na Urusi.
Matukio haya yanarudisha kumbukumbu ya vita
baridi kati ya mataifa hayo ambavyo vilidumu kwa zaidi ya miongo mitatu.
Katika miaka ya 60 hadi ile ya 80 karibu
ulimwengu mzima ulijipata umenaswa katika vita hivyo baridi na matai.
Mataifa hayo mawili yalikuwa yanang'aninia kuwa na ushawishi na hata
udhibiti wa karibu mataifa yote duniani.
Na ili kufanikisha kampeni zao serikali ya
Marekani na ile ya muungano wa Usovieti ziliwaweka majasusi karibu kote
duniani. Na sasa takriban miaka 20 tangu vita hivyo kukoma mbinu hizo
hizo bado zinaendelea kutumiwa.
0 comments:
Post a Comment