Jina la msichana wa miaka 6 wa Kimarekani limo katika orodha ya magaidi
Familia moja ya
Ohio nchini Marekani imepigwa na mshangao mkubwa wakati iliposikia kuwa
binti mdogo wa miaka 6 wa familia hiyo yumo katika orodha ya magaidi ya
Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani.
Hayo yalitokea hivi
karibuni wakati familia hiyo ya Dkt. Santhosh Thomas ilipokuwa imepanga
kusafiri kwa ndege kutoka Cleveland hadi Minneapolis.
Baada ya kuambiwa kuwa binti yake Alyssa Thomas hawezi kusafiri kwa ndege kwa sababu jina lake limo katika orodha ya magaidi, Dkt. Thomas alisema kwa istihzai kwamba:
"Wamesema, ‘Naam, yumo katika orodha.' Tumeshasikia, sawa, sasa uzito uko wapi? Twambieni tufanye nini ili tumtoe katika orodha hiyo, orodha hiyo siyo kabisa tunayotaka tuwemo ndani yake."
"Hivi hamumuoni hiki ni kibinti cha miaka 6 tu, hakitishii chochote," aliendelea kusema.
Ameongeza kuwa, "Pengine amewahi kumtishia mdogo wake wa kike, lakini sidhani kuwa hilo ni tishio linaloweza kuwashughulisha maafisa wa Wizara ya Usalama wa Ndani."
Hatimaye familia hiyo iliruhusiwa kusafiri kwa ndege kwa sharti kwamba baba wa familia hiyo aende akaripoti kwa Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani.
Baada ya kutokea mashambulizi ya Septemba 11, 2001, George W. Bush Rais wa wakati huo wa Marekani alibuni wizara mpya ya usalama wa ndani na hivyo kuzifanya wizara za nchi hiyo kuwa 14.
http://kiswahili.irib.ir/

0 comments:
Post a Comment