Rais Joseph Kabila wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo
Wakongomani wajkiandaa kuadhimisha
miaka 50 tangu walipojipatia uhuru wao kutoka Ubeligiji
Mfalme Albert II wa Ubeligiji na viongozi wengine wa kimataifa
wataadhimisha hapo kesho miaka 50 tangu Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo
ilipojikomboa toka enzi za ukoloni, ingawa nchi hiyo tajiri kwa maadini
ya kila aina imekabwa tangu wakati huo na miongo ya vita, rushwa na
umaskini.
Wimbo wa taifa la Kongo ulioimbwa kwa mara ya kwanza June 30 mwaka
1960 unawahimiza wananchi "wanyanyuke na kuijenga nchi kwa amani ili
izidi kupendeza kuliko zamani." Matumaini hayo lakini, yametoweka vibaya
sana.
Utawala wa miaka 32 wa Mobutu Sese Seko, aliyeingia madarakani mwaka
1965, uliikamua sana Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Ingawa ina akiba kubwa ya madini ya dhahabu, shaba, kobalt na
alamasi, Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ni moja wapo ya nchi maskini
kabisa za dunia, nchi iliyoathirika na vita vya miaka minane vya wenyewe
kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2003 na kugharimu maisha ya watu
wasiopungua milioni tatu.
Miaka minne baada ya Joseph Kabila kuchaguliwa kuwa rais, imesaidia
kuleta utulivu kidogo. Hata hivyo, thuluthi mbili ya wakongomani milioni
60 bado wanalazimika kuishi kwa dala moja na senti 25 kwa siku.
Maaskofu wa Kongo wameandika katika risala yao ya pamoja kuadhimisha
miaka 50 ya uhuru kwamba "Ndoto ya Congo inayopendeza imevurugwa".
"Kwa maoni yetu, Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imerejea nyuma
badala ya kusonga mbele," wamesema wachamungu hao.
Ziara ya mfalme Albert wa Pili ni ya kwanza kuwahi kufanywa na
mfalme wa Ubeligiji katika koloni lake hilo la zamani tangu miaka 25
iliyopita. Atajiunga na katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-Moon,
na rais Jacob Zuma wa Afrika kusini katika maadhimisho ya uhuru hapo
kesho mjini Kinshasa.
Afrika kusini imezitaja sherehe hizo kuwa ni "tukio muhimu kwa bara
lote la Afrika. Hata hivyo, viongozi wa Afrika kusini wameelezea wasi
wasi wao kwa kushindwa rais Kabila kurejesha utulivu katika eneo la
mashariki la nchi hiyo.
Wakinamama
walioyapa kisogo maskani yao wamewekwa katika kambi ya Kibati
Ziara ya mfalme Albert II na waziri mkuu aliyejiuzulu, Yves Leterme,
inabainisha uhusiano ulioanza upya kuwa mzuri kati Ubeligiji na koloni
lake hilo la zamani. Uhusiano huo ulipooza kufuatia lawama za rushwa
zilizotolewa na waziri mmoja wa Ubeligiji dhidi ya Jamhuri ya
kidemokrasi ya Kongo.
Mfalme Albert wa pili na Vyes Leterne hawapangi kusema chochote
hadharani wakati wa ziara hiyo ya siku nne iliyoanza jana usiku mjini
Kinshasa. Hata katika karamu ya chakula cha usiku hii leo, mfalme Albert
II hajapangiwa kuwahutubia viongozi wa mataifa ya kigeni
watakaohudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Jamhuri ya kidemokrasi
ya Kongo.
Na hata katika gwaride la kijeshji la kesho, mfalme Albert II
anatazamiwa kuvaa suti tuu badala ya sare ya kijeshi, ingawa yeye
binafsi ana cheo cha luteni jenerali na naibu amiri jeshi nchini mwake.
Mfalme Albert wa pili atatumia ziara yake hiyo ya siku nne, miongoni
mwa mengineyo, kuitembelea hospitali ya mfalme Baudoin pamoja na shule
mjini Kinshasa.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Afp,Reuters
0 comments:
Post a Comment