Serikali ya Burundi kupitia
mawaziri wa ulinzi na usalama wa raia imetoa onyo kali kwa muungano wa
vyama kumi na tatu vya upinzani vilivyopinga matokeo ya uchaguzi wa
madiwani uliofanyika tarehe 24 mwezi uliopita wa Mei.
Serikali imetangaza kwamba vikosi vya usalama
havitomvumilia yeyote yule anayekusudia kuzusha vurugu nchini Burundi.
Onyo hilo la serikali linafuatia habari kwamba
vyama hivyo vina mpango wa kuhujumu usalama nchini Burundi.
Hapo jana wagombea urais watano walitangaza
kutoshiriki katika uchaguzi huo wa urais wakidai kuwa chama tawala
kinapanga kuiba kura.
Lakini chama chama tawala cha rais Pierre
Nkurunziza kimepinga madai hayo na kusema, watano hao wanaogopa
kushindwa.
Miongoni mwa viongozi hao waliojiondoa ni pamoja
na aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la National Liberation Forces,
FNL, Agathon Rwasa ambaye angelikuwa mpinzani mkuu wa rais Nkurunziza.
Wiki iliyopita watano hao waliitisha kuvunjiliwa
mbali ya tume ya uchaguzi baada ya uchaguzi wa udiwani uliokamilika
tarehe 24 mwezi uliopita.
BBC Swahili
BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment