Serikali ya Israel, imeanza
shughuli ya kuwarejesha nyumbani kikundi cha kwanza cha mamia ya raia wa
kigeni waliokamatwa Jumatatu wiki hii, kwenye meli sita zilizokuwa
zimebeba bidhaa na chakula cha msaada kuelekea Gaza.
Wanaharakati tisa waliuawa wakati wa operesheni
hiyo. Mamia ya wanaharakati wa Kiarabu kutoka Palestina, walipelekwa
kwenye mpaka wa Israel na Jordan ambako watu wengi walikuwa wanasubiri
kuwalaki.
Israel pia imewaachilia huru raia 200 wa
Uturuki ambao wanatarajiwa kurejeshwa nyumbani.
Ripoti zinasema kwamba serikali ya Nchi hiyo,
inalenga kuwaachilia huru raia wote wa kigeni waliokuwa wakizuiliwa
gerezani katika kipindi cha saa 48 zijazo.
Afisa mmoja mwandamizi katika wizara ya mambo ya
nje ya Uturuki, Selin Yemel, amesema uamuzi huo unaonyesha kuwa
serikali ya Israel imetambua kosa lake.
Lakini msemaji wa serikali ya Israel amekariri
kuwa marufuku dhidi ya meli kuelekea eneo la Gaza bado itaendelea
kudumishwa, ili kuzuia silaha kusafirishwa hadi eneo hilo.
BBC Swahili
BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment