Wizara ya elimu ya China
imeanzisha mradi wa ushirikiano kati ya vyuo vikuu vya China na Afrika,
ili kutekeleza kihalisi Mpango wa utekelezaji wa Sharm el Sheikh
uliopitishwa kwenye mkutano wa 4 wa mawaziri wa baraza la ushirikiano
kati ya China na Afrika, uliofanyika mwaka jana nchini Misri.
Kwa mujibu wa mradi huo, vyuo vikuu 20 vya China na vingine 20 vya Afrika vitafanya ushirikiano, ambapo vyuo vikuu vya China vitatoa mafunzo ya kichina na mafunzo mengine kwa wanafunzi wa Afrika, na kutoa udhamini wa masomo.
Naibu waziri wa elimu wa China Bw. Hao Ping amesema mradi huo ni njia mpya China ya kuisaidia Afrika.
China Radio
Msemaji wa jeshi la Uganda, Luteni Kanali Felix Kulayigye amenukuliwa na Shirika la Habari la Ujerumani DPA, akisema kuwa wapiganaji hao wa LRA waliuawa wiki iliyopita.
Amesema kuwa jeshi la Uganda linaendelea kuwasaka wapiganaji hao wa LRA ambao wamekimbilia katika misitu ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Serikali za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Afrika ya Kati pamoja na Uganda zilitilia saini makubaliano ya kuwasaka waasi hao wa LRA.
Deutsche Welle
Kwa mujibu wa mradi huo, vyuo vikuu 20 vya China na vingine 20 vya Afrika vitafanya ushirikiano, ambapo vyuo vikuu vya China vitatoa mafunzo ya kichina na mafunzo mengine kwa wanafunzi wa Afrika, na kutoa udhamini wa masomo.
Naibu waziri wa elimu wa China Bw. Hao Ping amesema mradi huo ni njia mpya China ya kuisaidia Afrika.
China Radio
Waasi 16 wa LRA wauawa-KAMPALA
Jshi la Uganda limesema ,limewaua waasi 16 wa kundi la Lord´s Risistance Army LRA, katika mapambano yaliyotokea Jamuhuri ya Afrika ya Kati.Msemaji wa jeshi la Uganda, Luteni Kanali Felix Kulayigye amenukuliwa na Shirika la Habari la Ujerumani DPA, akisema kuwa wapiganaji hao wa LRA waliuawa wiki iliyopita.
Amesema kuwa jeshi la Uganda linaendelea kuwasaka wapiganaji hao wa LRA ambao wamekimbilia katika misitu ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Serikali za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Afrika ya Kati pamoja na Uganda zilitilia saini makubaliano ya kuwasaka waasi hao wa LRA.
Deutsche Welle
0 comments:
Post a Comment