SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, June 29, 2010



Mr II aachiwa kwa dhamana jana baada ya kukamatwa
MSANII wa Kizazi Kipya, Joseph Mbilinyi, al maarufu kama Mr II jana alikamatwa kama tulivyoeleza awali, na kushikiliwa kwa zaidi ya masaa matano na Jeshi la Polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutishia kuua kwa kutumia muziki wake.
Mr II alikumbwa na mkasa huo majira ya saa tano asubuhi kwenye viunga vya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), wakati akijiandaa kuwasilisha mada ya Muziki wa bongo fleva ulipotoka na hatma yake kwenye jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye ukumbi wa Baraza hilo.
Globu ya Jamii ambayo imeshuhudia Mr II akiwa chini ya ulinzi Makao Makuu ya Jeshi 'Wizara ya Mambo ya Ndani' kwa mahojiano. Hata hivyo jeshi hilo halikuwa tayari kutoa taarifa zozote kwa madai kuwa upelelezi bado unaendelea na utakapokamilika utaweka wazi suala hilo.
Hata hivyo habari kutoka kwa watu wa karibu na Mr II zinasema kuwa mwanamuziki huyo aliitwa kwa mahojiano tangu Alhamisi iliyopita na watu walinzi hao wa usalama wa raia lakini hakuitikia wito.
Inadaiwa Mr II amesambaza CD yenye nyimbo 14 aliyoipa jina la "Anti Virus Mix Tape" ambayo amekikashifu kituo kimoja cha redio ikiwa ni pamoja watangazaji na wakurugenzi wa kituo hicho.
Katika CD hiyo Mr II ameshirikiana na wasanii zaidi ya 10 akiwemo kama G – Solo, Mapacha na Mkoloni.
Akizungumza na Blog ya Jamii mara baada ya kuachiwa kwa dhamana majira ya saa 11 jioni Mr II alisema: “Nashukuru nimeachiwa kwa dhamana.
"Nimejidhamini mwenyewe. Nchi hii ina uonevu sana. Eti wanasema wamenikamata kwa tuhuma za kutishia kuua kwa maneno kwa kutumia mziki wangu.
"Wameniambia niripoti tena Polisi siku ya Jumatano kwa mahojiano zaidi na kwamba upelelezi wao bado unaendelea.”alisema Mr II.
issamichuzi blog

0 comments:

Post a Comment