Wizara ya mambo ya ndani ya
Uingereza, kwa mara ya kwanza imeweka kikwazo kuhusu idadi ya wahamiaji
kutoka nje ya Umoja wa Ulaya watakaoruhusiwa kuingia nchini humo.
Waziri wa mambo ya ndani,Theresa May amesema
hatua hiyo ni katika juhudi za kupunguza idadi ya wahamiaji hadi
itakapofikia jinsi ilivyokuwa miaka ya tisini.
Ni wafanyikazi elfu ishirini na nne pekee kutoka
nje ya Umoja wa Ulaya watakaoruhusiwa kuingia nchini Uingereza kati ya
sasa na mwezi Aprili, mwaka ujao ambapo serikali inapanga kuanzisha
sheria mpya ya kudhibiti wahamiaji.
Serikali bado haijasema sheria hiyo mpya
inalenga kupunguza idadi ya wahamiji kwa kiwango gani.
Idadi ya wahamiaji nchini Uingereza imeripotiwa
kuongezeka kwa kasi zaidi katika miaka ya hivi karibuni.
Hatahivyo,hatua ya serikali ya Uingereza
kupunguza idadi ya wahamiaji haijashabikiwa na viongozi wa kibiashara na
kisiasa, ambao wameikosoa vikali, wakisema itaathiri uchumi wa nchi na
haitachangia kwa njia yoyote katika kupunguza wahamiaji haramu.
Wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika hivi
karibuni,kura ya maoni ilionyesha kuwa uhamiaji na uchumi ndiyo
yalikuwa maswala muhimu zaidi kwa wapigaji kura, huku wengi wao
wakilalamika kuwa idadi ya wahamiaji imeongezeka sana.
0 comments:
Post a Comment