SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, April 7, 2016

TASWIRA MBALIMBALI ZA RAIS MAGUFULI NA RAIS KAGAME WAKIWA NCHINI RWANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Bi Tonia Kandiero, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la Rusumo linalounganisha nchi za Rwanda na Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiweka jiwe la ufunguzi la kituo cha pamoja cha huduma za mpakani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha pamoja cha huduma za mpakani.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa daraja la Rusumo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Rusumo mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Bi Tonia Kandiero, pamoja na Balozi wa Japan Masaharu Yoshida pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakipita kwenye Daraja la Rusumo mara baada ya ufunguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwasili kwenye ardhi ya nchi ya Rwanda na kulakiwa na kikundi cha ngoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kutoa hotuba yake kwa upande wa Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Kagame katika mazungumzo rasmi baina ya nchi hizo mbili nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Rusumo mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakielekea jukwaani mara baada ya kuwasili Rusumo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakizungumza jambo kabla ya ufunguzi wa daraja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika eneo la Rusumo Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya ukaguzi wa kituo cha pamoja cha huduma za mpakani huku Rais wa Rwanda Paul Kagame akifurahia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia upande wa Rwanda katika eneo la Rusumo. Picha na IKULU

0 comments:

Post a Comment