SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 2, 2016

NAPE AWAASA KAMATI YA MAUDHUI KUELIMISHA WADAU WAKE

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipewa maelekezo jinsi mtambo wa usimamizi wa masafa unavyofanya kazi katika ofisi za mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA).Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dk.Ally Simba.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Posta wa TCRA Bw.Haruni Lemanya jinsi mitambo ya mawasiliano ya kizamani iliyowekwa katika makumbusho ya mawasiliano iliyopo katika ofisi za mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA).Kulia kwake ni ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dk.Ally Simba akifatilia kwa karibu.
 Naibu MKurugenzi Idara ya Utangazaji(TCRA)Bw.Frederick Ntobi akieleza jambo kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye jinsi uangalizi wa maudhui ya Utangazaji yanavyofanyika na mamalaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dk.Ally Simba na Meneja mawasiliano wa mamalaka hiyo Bw.Innocent Mungy(wa kwanza kulia).
 Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dk.Ally Simba(katikati) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye jinsi kituo cha usimamizi wa mawasiliano kinavyofanya kazi katika mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dk.Ally Simba(wa kwanza kulia) na wajumbe wa kamati ya maudhui ambao ni mwenyekiti wa kamati hiyo margareth munyagi(wa tatu kushoto),Abdul Ngarawa(wa nne kulia)Joseph Mapunda(wa pili kulia),Zainabu Mwatawala(wa tatu kulia) na Derek Murusuri(wa pili kulia).

Picha na Daudi Manongi-WHUSM.

Na Zawadi Msalla-WHUSM.

Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nnauye  amewaasa wajumbe wa kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kujenga mazoea ya kuelimisha Umma badala ya kusubiri makosa ili waweze kutoa adhabu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye alipokuwa akizindua kamati hiyo ya Maudhui leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Alisema ni vema kama wadau wakuu wakafahamu majukumu ya kamati hiyo na kuelimishwa nini wanachopaswa kukifanya ili kuzuia baadhi ya makosa ambayo yangeweza kuzuilika na kuongeza kuwa kinga ni bora kuliko tiba.

Katika uzinduzi wa kamati hiyo pia alitoa wito wa kuangalia jinsi ambavyo vyombo vya habari wanazingatia sheria ya matumizi ya asilimia sitini ya maudhui ya Kitanzania katika vipindi vyao kwani suala hilo bado lina lalamikiwa na wadau wengi.
“ Najua kuna ugumu wa kuisukuma hiyo sheria, ila isimamiwe vizuri,takwimu hazifurahishi sana na kama inaonekana sheria hiyo haitekelezeki ni bora iangaliwe kwa upya” alisema waziri.

Kwa upande wake mjumbe wa Kamati hiyo Bw. Joseph Mapunda alisema kuwa licha ya umakini watakao kuwa nao katika kutekeleza majukumu yao Kamati imedhamiria kuhakikisha inahamasisha suala la mafunzo kwa watangazaji yanatiliwa mkazo kwani watangazaji wengi hawana mafunzo bora ya utangazaji.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya watangazaji  nchini wafanya kazi katika mazingira magumu inayopelekea utendaji usio na tija, hivyo kamati yao itafanya ushawishi kuhakikisha wanathaminiwa na kufanya kazi katika mazingira rafiki.

0 comments:

Post a Comment