SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, April 4, 2016

Hivi Unajua Madhara Ya Utumiaji Wa Shisha? - Dr. Sajjad Fazel Mtaalamu Wa Madawa Tiba Azungumzia

 Dr. Sajjad Fazel,Mtaalamu wa Madawa Tiba azungumzia madhara ya Utumiaji wa Shisha.
Dr. Sajjad Fazel ni Mtaalamu wa Madawa Tiba amezungumza kwenye kipindi cha Clouds360 cha Clouds TV kuhusu madhara ya Shisha hasa kwa vijana ambao ndiyo watumiaji wa kubwa.
12512740_233277127026319_7091801581589609580_n[2]

Alisema tofauti ya Shisha na Sigara ni kuwa tumbaku iliyowekwa kwenye Sisha imeongezewa ladha (Flavour) mbalimbali kama mchungwa nyingine.
Mtumiaji huvuta Shisha kwa nusu saa na zaidi, akivuta kwa saa nzima ni sawa na mtu aliyevuta sigara 100 kwa siku. Moshi wa sigara ukivuta kwa saa nzima ni nusu lita ila shisha kwa saa nzima ni lita 90.
Hivyo hii inafanya shisha kuwa hatari zaidi kuliko sigara. Watu hujidanganya kuwa maji kwenye shisha huondoa Nicotin na Kemikali zinazosababisha Saratani kitu ambacho sio kweli.
Mkaa unaotumika kuchomea shisha nao huongeza kemikali ambazo mvutaji huziingiza ndani ya mwili ambazo ni hatari.
Dr. Sajjad aliekeza kuwa sababu kubwa zinazowafanya vijana kuvuta shisha sana ni:- 1. Vijana wengi hudhani shisha haina madhara kama ilivyo sigara.
  1. Ladha za matunda ambazo huwekwa kwenye shisha.
  2. Shisha huvutwa watu wakiwa pamoja, hivyo huwa wanavuta huku wanapiga story na kama kuna ambaye havuti hushawishika kuvuta.
Akiendelea kueleza madhara hayo Dr. Sajjad alisema, Moshi wa shisha huleta madhara kwa mtu aliekaa karibu na mvutaji kuliko hata mtu anayevuta sigara anavyoathirika. Bomba moja linalotumiwa na wavutaji licha ya kubadilisha mpira wa juu wa kuvutia huweza kusababisha magonjwa kama TB, Limonia na Flu.
Alisema, nchi nyingine zimeweza kupunguza idadi ya watumiaji na watu wanaoathirika na shisha, kwanza kwa kuondoa ladha kwenye shisha ambayo ndio huwavutia wengi, wameweka picha ya mapafu yaliyoathirika ili kuwaonyesha watumiaji uhalisia wa athari na pia kuweka naeneo maalum kwa ajili ya kuvutia shisha na sigara (Smoking Zone) ili ambao hawavuti wasiathirike.
Akimalizia mahojiano alisema, Shisha pekee haipelekei mtu kutumia dawa za kukevya labda kama mtumiaji ataanza kuchanganya na bangi au dawa nyingine. Pia Dr. Sajjad aliwataka watanzania kuwa wanasoma makala zake kwenye gazeti la #TheGuardian kila jumamosi ambapo ameahidi kuendelea kuandika zaidi juu ya madhara ya shisha
CHANZO : BOFYA HAPA

0 comments:

Post a Comment