SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, April 4, 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA, DK KIGWANGALLA AZINDUA RASMI MAJENGO YA T-MARC TANZANIA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akikata utepe wakati wa kuzindua jengo la ofisi la kampuni ya T-MARC Tanzania, Kulia ni  Mkurugenzi mtendaji wa T-MARC Tanzania,Diana Kisaka na kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T-MARC, Charles Singili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifungua rasmi jengo la ofisi ya T- MARC Tanzania
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufanya uzinduzi wa majengo ya kampuni ya T-MARC Tanzania
Wafanyakaiz wa T-MARC Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa majengo mawili kumalizika.
Mgeni rasmi akisubiriwa kulizindua jengo hilo.
 Mkurugenzi mtendaji wa T-MARC Tanzania,Diana Kisaka(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Ofisi pamoja na jengo la kuhifadhia mali za kampuni ya T-MARC Tanzania, Kulia ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya  T-MARC, Charles Singili (katikati)
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T -MARC, Charles Singili(katikati)  akizungumza na waandishi wa habari wakatinwa hafla ya uzinduzi wa jengo la ofisi pamoja na ghala la kuhifadhia mali za kampuni.
 Meneja Mradi wa asasi ya T-MARC Tanzania, Doris Chalambo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi wa majrngo ya kapuni ya T-Marc Tanzania
Mmoja wa Wasanii kutoka kundi la Wanne Star akionesha umahiri wake wa kucheza kwa staili ya aina yake kiasi hata cha kuwavutia wahudhuriaji waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa majengo ya kampuni ya T-MARC Tanzania
Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Diana Kisaka(katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu shughuli wanazozifanya katika kampuni ya T-MARC Tanzania mara baada ya kuwasili kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya T Mark, Charles Singili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa T-MARC Tanzania alipotembelea mabanda ya kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa majengo ya kampuni hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya T-MARC Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi
kumalizika

0 comments:

Post a Comment