MGOGORO wa uongozi ndani ya Chama
cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) umeingia katika hatua tata baada
ya viongozi waanzilishi wa chama hicho kulalamikia uchaguzi uliopangwa
kufanyika Mai 30, 2015 mjini Dodoma ilhali kuna mgogoro wa uongozi ndani
ya chama hicho ukiendelea.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi kwa niaba ya viongozi wenzake Mwenyekiti wa TAPSEA, Pili Mpenda
ambaye pia ni miongoni mwa waanzilishi wa chama hicho jana jijini Dar es
Salaam alisema anasikitishwa na kitendo cha viongozi walioingia kinyume
na katiba ya chama hicho kujipanga kufanya uchaguzi ilhali kuna kesi ya
msingi ipo mahakamani kulalamikia wao kuondolewa madarakani.
Alisema viongozi waliopo
madarakani sasa wameingia kwa nguvu za Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
baada ya kushinikiza uchaguzi kinyume na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa
kwanza wa TAPSEA uliofanyika Arusha Mai 18, 2013 wa chama hicho ambao
ulielekeza maboresho ya katiba ya chama kabla ya chochote kufanyika.
Alisema mkutano mkuu wa pili
uliofanyika mkoani Mwanza 2014 uliitishwa ili kuwaeleza wananchama juu
ya shinikizo la msajili na wanachama wachache (7) kufanyika uchaguzi na
kuwaeleza mwenendo wa marekebisho ya katiba ya TAPSEA lakini Ofisa
msajili alishinikiza ufanyike uchaguzi ambao uliwagawa wanachama na
wengine kususia uchaguzi huo kutokana na mvutano.
Bi. Mpenda alisema uchaguzi
uliofanyika haukuwa halali kwani mbali na kufanyika kinyume na katiba ya
TAPSEA na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa kwanza haukushirikisha wanachama
wote. Aliongeza kuwa kati ya wanachama halali 815 waliokuwa
wamejisajili ni wanachama 200 tu ndio walioshiriki katika uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment