Wageni wakijichagulia bidhaa za Tanzania wakati wa sherehe hizo.
Dada Tabia Mwanjelwa (mwenye) gitaa akiwa na wasanii wenzie jukwaani.
Msanii John Gambula na Tadeo Simon, wakiwa na watoto jukwaani.
Wasanii wa kikundi cha Wabantu wakiipeperusha TZ.
Dada Tabia Mwanjelwa (mwenye gitaa) akiwa na wasanii wenzie jukwaani.
Siku ya Jumamosi 27.04.2013 Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani,
chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno
"MUUNGANO" lina maana kamili kwa maisha ya Mtanzania na binadamu
wengine.
Sherehe hizo zilizowakusanya Watanzania na marafiki waTanzania kutoka kila kona ya Ujerumani, ziliutingisha mji wa Koloni katika usiku usio kwisha wa kusherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Ali Siwa, Naibu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikuwa mstari wa mbele akiwaongoza Watanzania katika Muungano Day.
Wasanii mbalimbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tanzania. Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Mfundo na kamati yake wameahidi kufanya mambo makubwa na kuitangaza Tanzania kwa hali na mali chini ya Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU).

0 comments:
Post a Comment