Wachezaji wa Sevilla wakisherehekea na Kombe la Europa League jana Uwanja wa Taifa wa Warsaw, Poland.
SEVILLA
ya Hispania imefanikiwa kutetea Kombe la Europa League baada ya kutoka
nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya Dnipro usiku wa kuamkia leo katika
mchezo wa fainali uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Warsaw. Poland.
Nikola
Kalinic alianza kuifungia Dnipro dakika ya saba, kabla ya Sevilla
kuzinduka na kupata mabao mawili ya haraka kupitia kwa Grzegorz
Krychowiak na Carlos Bacca ndani ya dakika tatu.
Nahodha
wa Dnipro, Ruslan Rotan akaifungia timu hiyo ya Ukraine bao la
kusawazisha kwa shuti la mpira wa adhabu kaba ya mapumziko na Bacca
akafunga bao lake la pili katika mchezo huo na la ushindi kwa Sevilla
dakika ya 73.
Kwa
matokeo hayo, Sevilla itacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada
ya kutetea taji la Europa League. Beki wa Dnipro, Matheus alipoteza
fahamu baada ya kugongana kichwani na Benoit Tremoulinas.
Kikosi
cha Sevilla kilikuwa; Rico, Vidal, Kolodzjejczak, Carrico, Tremoulinas,
Krychowiak, Mbia, Banega/Iborra dk87, Reyes/Coke dk58, Vitolo,
Bacca/Gameiro dk82.
Dnipro;
Boyko, Fedetskyi, Douglas, Cheberyachko, Leo Matos, Kankva/Shakhov
dk85, Fedorchuk/Bezus dk68, Matheus, Rotan, Konoplyanka na
Kalinic/Seleznyov dk78.
Na BinZubeiry
Na BinZubeiry
0 comments:
Post a Comment