Balozi
Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dr. Ali Mohammed Shein akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa
Mabalozi wa Tanzania uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Ramada Mjini
Dar es Salaam.Baadhi
ya Mabalozi wa Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani walioshiriki
Mkutano wao wakifuatilia Hotuba ya Ufungaji wa Mkutano huo iliyosomwa
na Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. ASli Mohammed Shein.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Tanzania Nchi mbali mbali Duniani mara baada ya kufunga Mkutano wao wa Nne ulifanyika Ramada Hoteli Jijini Dar es Salaam. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Bernard Membe, Katibu Mkuu Mpya wa Wizara hiyo Balozi Lebereta Mula mula na kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mhadhi Juma Maalim. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Jamuhuri ya Watu wa China Balozi Abrahaman Nyimbo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania Mjini Dar es salaam. Picha na – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Tanzania Nchi mbali mbali Duniani mara baada ya kufunga Mkutano wao wa Nne ulifanyika Ramada Hoteli Jijini Dar es Salaam. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Bernard Membe, Katibu Mkuu Mpya wa Wizara hiyo Balozi Lebereta Mula mula na kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mhadhi Juma Maalim. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Jamuhuri ya Watu wa China Balozi Abrahaman Nyimbo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania Mjini Dar es salaam. Picha na – OMPR – ZNZ.
---
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein
alisema Mabalozi wanayoiwakilisha Tanzania katika Mataifa tofauti
Duniani wanapaswa kuitekeleza vilivyo Sera ya Mambo ya Nje inayolenga
katika Diplomasia ya uchumi ambayo ndiyo muongozo wao katika utekelezaji
wa jukumu lao la msingi.
Alisema
Sera hiyo ni vyema ikatumika vizuri wakati huu ambao Taifa la Tanzania
linatekeleza Dira ya kuelekea uchumi wa Kati na kati ifikapo mwaka 2020
kwa upande wa Zanzibar na Mwaka 2025 kwa Tanzania Bara.
Dr.
Ali Mohammed Shein alisema hayo wakati akiufunga Mkutano wa Nne wa siku
Tatu wa Mabalozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Hotuba
iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ramada Jijini Dar es
Salaam.
Alisema
katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi ya utekelezaji wa Sera ya Mambo
ya Nje yenye kuweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi Tanzania
imepiga hatua kubwa vikiwemo Visiwa vya Zanzibar.
Dr.
Shein alifahamisha kwamba matunda ya Sera hii yanadhihirisha wazi
ukuaji wa sekta ya Utalii, miradi mengine ya kiuchumi ikiwemo pia ile
mikubwa inayotekelezwa na wahisani kwa upande wa Zanzibar.
“
Mikakati mipya ya muda mfupi na mrefu mliowekeana katika Mkutano huu ni
msingi mzuri kabisa kufuatana na mabadiliko ya uchumi yanayotokea
Duniani na kufikia malengo ya Dira ya 2020 na 2025 “. Alisema Dr. Shein.
“
Nina hakika kuwa katika Mkutano huu mmeweza kuziba nyufa zote
zilizojitokeza katika utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001
inayolenga katika Diplomasia ya Uchumi ambayo ndio muongozo wetu katika
utekelezaji wake na ni jukumu letu la msingi “. Alisisitiza Dr. Shein.
Rais
wa Zanzibar alieleza kwamba licha ya mafanikio makubwa ya kiuchumi na
maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa kwa upande wa Zanzibar lakini bado
iko haja kwa Mabalozi hao wa Tanzania kuongeza juhudi za kuitangaza Zanzibar katika Mataifa waliyopangiwa kutekeleza majukumu yao ya Kidiplomasia.
Alisema
mafanikio ya Zanzibar katika kukuza sekta ya Utalii , uwekezaji na
utekelezaji wa mipango mengine ya maendeleo hutegemea sana juhudi za
Ofisi za Kibalozi katika kuitangaza Zanzibar nchi za Nje.
Dr.
Shein alifahamisha kwamba baadhi ya wakati Serikali imekuwa
ikipokea malalamiko kutoka kwa wawekezaji, watalii na wageni wanaofika
Zanzibar juu ya ukosefu wa taarifa za kutosha kuhusu Zanzibar katika
Ofisi za Kibalozi za Tanzania.
Aliwakumbusha
Mabalozi hao kwamba katika kutekeleza majukumu yao ni vyema kila wakati
wakazingatia kuwa Ofisi zao zinaweka taarifa za kutosha juu ya sekta
zote muhimu za kiuchumi na kijamii za pande zote mbili za Jamuhuri hasa
zile fursa za uwekezaji vivutio vya utalii.
“
Suala hili nimekuwa nikilikumbusha kila ninapopata fursa ya
kuzungumza nanyi, hasa wakatia mbao Mabalozi huja kunitembelea na
kuniaga kabla ya kuripoti katika vituo vyao vya kazi “. Alifafanua Dr.
Shein.
Alifahamisha
kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kupokea mawazo ya
Mabalozi hao ili kupata fursa nzuri ya nini Wanadipomasia
hao wakitangaze kuhusu Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar alihimiza kwamba katika kipindi hichi ambapo Nchi
mbali mbali Duniani zimekumbwa na misukosuko ya kutetereka kwa hali ya
amani na utulivu Mbalozi hao wanapaswa kuzitangaza fursa ya kiuchumi
zilizopo Nchini na kuzihusisha na hali ya amani na utulivu uliopo Nchini
Tanzania.
Alieleza
kuwa amani na utulivu ni miongoni mwa vigezo muhimu vya awali
vinavyozingatiwa na wawekezaji pamoja na wageni wanaotaka kwenda nje ya
nchi zao kwa nia ya kuwekeza na kufanya biashara.
Mapema
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mh.
Bernard Membe alisema utekelezaji wa sera ya mambo ya nje inayolenga
katika Diplomasia ya Uchumi umeleta faida kubwa katika uchumi wa Taifa
ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Waziri
Membe alisema ipo miradi kadhaa ya kiuchumi iliyotokana na sera hiyo
kufuatiwa kutanganzwa na Ofisi za Kibalozi za Tanzania akiitaja kuwa ni
pamoja na misaada ya maendeleo iliyofadhiliwa na mpango wa Milenia wa
Marekani MCC na mradi wa chuma wa Mchuchuma.
Mh.
Membe alisisitiza pia kuwa ipo miradi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo,
Tanzania kusamehewa mikopo tofauti kutoka kwa baadhi ya wafadhili,
mradi wa huduma za maji safi unafadhiiwa na Serikali ya Japan pamoja na
mradi wa Kilimo kwa upande wa Visiwa vya Zanzibar.
Alisisitiza
kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya
Mambo ya nje itahakikisha kwamba inaendelea kuchangia vikosi vya kulinda
amani Barani Afrika.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya washiriki wa Mkutano huo wa Nne wa Mabalozi wa
Tanzania Nchi Mbali mbali Duniani Dini wa Mabalozi hao Balozi Kijazi
alisema Maalozi hao wakirudi vituoni mwao watakuwa na kazi moja tu ya
kutekeleza yale waliyoyajadili na kukuibaliana katika Mkutano huo.
Balozi
Kijazi alilihakikishia Taifa kwamba Mabalozi hao wana nia safi ya
kutekeleza majukumu yao kwa ufasini uliotukuka, lakini lakuzingatia
zaidi ni uwezeshwaji wao ili kutekeleza vyema kazi yao hiyo ya
Kidiplomasia.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment