Mwigizaji
wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),akipewa maelekezo
ya kuendesha Trekta mara Baada kukabidhiwa ufunguo wake na Fundi
Mkuu wa Kampuni ya Farm Equip Tanzania , Yunusu Nsekela wakati wa
kukabidhiwa Matrekta kwaajili ya kilimo jijini Dar es Salaam leo
Mwakilishi
wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta
lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi
wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta
lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink akisalimiana
mara baada ya akimkabidhi ufungua wa Trekta lake Mwigizaji wa Origino
Komed, Isaya Mwakilasa(Wakuvanga) jijini Dar es Salaam leo.
Mwigizaji
wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee) akishukuru kwa
niaba ya waigizaji wa kundi la Origino Komedi mara baada ya kukabidhiwa
Funguo za Matrekta ya Kilimo jijini Dar es Salaam leo, kutoka kushoto
ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif
Sheink,Isaya Mwakilasa(Wakuvanga ),Lucacy Mhavile(Joti) na kulia ni Alex Chalamila(Mackregani).
Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink akizungumza
na Vijana wa Kundi la Origino Komedi mara baada ya kuwakabidhi
funguo za Matrekta ya kilimo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink , katika picha ya pamoja waigizaji wa kundi la Origino Komedi na nyuma yao ni Matrekta ambayo wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano ya Matrekta ya Kilimo kati ya Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink na
Waigizaji wa kundi la Origino Komedi, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Matrekta ya Kilimo ambayo waigizaji wa Kundi la Original Comedi
wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya
Jamii.
Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.
WAIGIZAJI
wa kindi cha Origino Komedi wamewaasa vijana kutumia vipaji vyao ili
kutengeneza maisha yao kuwa mazuri na sio kufikiri kuwa vijana wengi
hushikwa mkono na mtu ili kufanikiwa.
Hayo
yamesemwa na kundi la waigizaji wa Origino Komedi wakati wa kukabidhiwa
Matrekta ya Kilimo aina ya Sonalika kutoka kampuni ya Farm Equip
Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink amesema
kuwa vijana wameamua kufanya jambo la maana kwa jamii ,"kwani
wamenunua matrekta kwa ajili ya kilimo,vijana wengi wamekuwa wakinunua
magari ya kifahari bila kujua kunakesho na keshokutwa kwa maendeleo
yao",alisema Bwa Arif.
Nae
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewapongeza vijana wa kundi
hilo kuwa kufanya maamuzi sahihi na ya maendeleo kwa kununua Matrekta
hayo kwaajili ya kilimo,amesema kuwa uamuzi wao ni mzuri hata kwa jamii
kwani pia kwa namna moja ama nyingine itasaidia kuongeza ajira kwa
vijana,kwakuwa kilimo kinahitaji watu wengine na sio wao wenyewe watakao
weza kuendesha Matrekta hayo mashambani.
Kundi
hilo la Origino Komedi linaundwa na vijana 7 ambao ni Alex
Chalamila(Mackregani),Josef Shamba(Vengu),Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani
Mzee),Lucacy Mhavile(Joti), Isaya Mwakilasa(Wakuvanga),Emmanuel
Mgaya(Masanja mkandamizaji) na Davidi Seki.
Waigizaji hao wameahidi kupoleka Matrekta yao kwenda kubeba takataka katika Wilaya
ya Kinondoni ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda atazindua
kampeni ya Ona aibu, ambayo itahamasisha usafi katika Wilaya ya
Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment