SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 22, 2015

SIJAFUKUZWA UANACHAMA WA TLP-MREMA

Mwenyekiti   wa chama cha Tnzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo)   katika mkutano uiliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MELEZO kuhusu kukanusha  kuwa yeye amefukuzwa TLP,Kushoto Mkurugenzi wa Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo,Kulia ni Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mrikariya.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MWENYEKITI wa Chama cha Tnzania Labour Party (TLP) Agustino Mrema,amesema hajafukuzwa unachama katika chama hicho.

Mrema aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana kuwa yeye ni mwenyekiti wa Chama hicho na hakuna mtu wa kumtoa kutokana na kuendesha chama hicho kwa kufuata katiba.

Amesema kikundi kinachofanya hivyo na kusambaza taarifa kuwa kimemtoa kutokana na kufanya vikao hakitambui na kuwataka wanachama kuwabeza watu hao. 

Mrema amesema yeye akiwa Mwenyekiti ataendelea kutetea jimbo lake la Vunjo,hivyo watu wanaosema amefukuzwa katika chama wapuuzwe.
Aidha amesema biashara ya Urais ameachana nayo ,sasa kazi yake ni Ubunge kupitia jimbo la Vunjo na ameweza kuleta maendeleo ya wananachi katika jimbo hilo

0 comments:

Post a Comment