Balozi wa China nchini Tanzania,Mh. Lu Youqing akizungumza na vyombo vya habari mjini Arusha leo juu ya tuhuma za kuhusishwa kwa Ndege ya Rais wa China kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii,Mh. James Lembeli.
Serikali
ya China imelaani vikali uzushi uliotolewa na vyombo vya magharibi
kutuhumu ndege ya Rais huyo kutumika kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.
Akizungumza
leo mjini Arusha Balozi wa China Lu Youqing alisema kuwa huo ni uongo
mkubwa ambao ulikuwa na nia ya kutia aibu taifa lake na Tanzania kwa
ujumla.
Alisema
kwamba Taifa lake hutoa adhabu kali kwa mtu anayefanya uovu kama
ujangili, "Kama mwandishi angeweza kuthibitisha hao maafisa
wangechukuliwa hatua kali, na hilo liko ndani ya uwezo wangu kwanini
ameshindwa kuwataja?"
Lu
alisema kwamba Adhabu kama hiyo si kwa mtu aliyekutwa na nyara tu bali
hata kwa muongo, "Mwandishi huyo ni muongo na anatakiwa aadhibiwe".
Waziri
wa maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu aliunga mkono kauli hiyo na
kusema kuwa ilikuwa na nia ya kuchafua hali ya hewa kutokana na mkutano
wa kimataifa ulioanza leo jijini Arusha.
"Hata
tulipokwenda na rais Kikwete jijini London kwa mkutano wa kimataifa juu
ya ujangili gazeti la Dail Mail lilitoa habari za kashfa kuhusu
Tanzania siku moja kabla ya mkutano na hii leo ndio limetokea"
Alisema
nashukuru wadau wa uhifadhi ambao kwa kiwango kikubwa wamehudhuria
kikao chetu muhimu cha leo ambacho kitaleta mabadiliko makubwa katika
vita dhidi ya ujangili.
Kikao
hichio kilihudhuriwa na mawaziri kutoka nchi tisa za Afrika ukanda wa
bahari ya Hindi na afrika mashariki na Kati pamoja na wawakilishi wa
mashirika mbalimbali na balozi wa nchi nyingi wanaowakilisha nchi zao.
0 comments:
Post a Comment