SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, November 3, 2014

ManCity yaichapa Manchester United 1-0

Man City vs. Man United: Full Match Highlight and Player Ratings
Mchezaji wa Manchester City Sergio Aguero akishangilia goli katika ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester United
Manchester City imeendeleza ubabe wake dhidi ya majirani zao Manchester United kwa kuwachapa goli 1-0 katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa Etihad, Jumapili.
Sergio Aguero aliipatia timu yake goli hilo katika dakika ya 63 ya mchezo.
Goli hilo la kumi kwa Aguero katika msimu huu wa ligi kuu ya England liliivunja Manchester United iliyokuwa na ngome iliyosambaratika baada ya Chris Smalling kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza cha mchezo na Marcos Rojo kutolewa nje katika machela baada ya mapumziko kutokana na kuumia bega.

Chris Smalling wa Manchester United akionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Manchester City, Jumapili
Ushindi huu wa Manchester City pia unatoa mwanga wa matumaini kwa kocha Manuel Pellegrini ambaye wiki iliyopita, timu yake ilipoteza kwa West Ham katika mchezo wa ligi kuu na kisha kutolewa katika kombe la Capital One baada ya kufungwa nyumbani na Newcastle.
Manchester City walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo.
Mchezo kati ya Manchester City na Manchester United ulikuwa mpambano mkali, ukiwa wa kwanza kwa meneja mpya wa Manchester United, Louis van Gaal, akishuhudia ngome ya timu yake ikiyumba na nguvu ya safu ya ushambuliaji ya kina Angel Di Maria, Robin van Persie na Wayne Rooney ikishindwa kupeleka michomo iliyotarajiwa katika lango la Manchester City.
Wakati meneja wa Manchester United akisikitika kwa makosa ya kizembe yaliyomsababishia Chris Smalling kutolewa nje kwa kadi nyekundu, wenyeji Manchester City walijawa na furaha kwa kushinda kwa mara ya sita katika michezo saba iliyozikutanisha timu hizo na pia Manchester City ikishinda mechi nne mfululizo dhidi ya Manchester United.
Kwa matokeo hayo Chelsea bado inashikilia usukani wa ligi kuu ya England ikiwa na pointi 26, pointi sita juu ya Manchester City na pointi nne juu ya Southampton inayoshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.
Manchester United iko katika nafasi ya kumi baada ya michezo kumi ikiwa na pointi 13, huku Burnely ikiwa katika nafasi ya ishirini na ya mwisho katika ligi kuu hiyo, kwa kujikusanyia pointi nne tu katika michezo yake kumi iliyokwishacheza.

Chanzo:BBC

0 comments:

Post a Comment