Komredi Kinana akipandisha bendera wakati wa uzinduzi wa shina la Wakereketwa la CCM la Wanywaji wa Kahawa mjini Lindi Jana
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara
mjini Lindi jana, kuhitimisha ziara ya siku 8 katika Mkoa wa Lindi ya
kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa
kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza
kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa
hadhara mjini Lindi, ambapo amesema wapinzani wajiandae kupigwa mweleka
katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa Desemba 2014, akidai hawana mpango
wa kuwaletea maendeleo wananchi.Pia amesema Mbunge wa Jimbo la Lindi
Mjini Baruani wa CUF, ajiandae kung'oka akidai kodi yake imekwisha.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akishishiriki kuchimba miundombinu ya
maji katika Kijiji cha Mingoyo Mnazi Mmoja Lindi Mjini jana
Kinana
akiungana na wananchi kupapalia katika shamba la kuzalisha mbegu bora
za mihogo katika Kijiji cha Chikonji, wakati wa zaiara yake Wilaya ya
Lindi Mjini.
Kinana akisaidia kubeba zege za kujengea nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Nanyanje, Lindi Mjini.
Kinana akishiriki kuvua samaki katika moja ya mabwawa 12 ya mjasiriamali Mjini Lindi
Komredi Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Lindi jana
Kikundi cha Mangongoti kikitumbuiza katika mkutano huo
Komredi Kinana akiwapongeza vijana wa Chuo cha Veta walioujiunga na Umoja wa Vijana wa CCM wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Ally Mtopa akihutubia kabla ya kumkaribisha Kinana wakati wa mkutano huo.
Kinana akihutubia umati mkubwa wa wananchi mjini Lindi leo
Kinana akiwapatia kadi za CCM wanachama waliohama kutoka vyama vya upinzani
Mwanachama wa CUF kwa miaka 18, Omari Kalunda akitangaza kuachana na chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Ally Mtopa akimzawadia mgolole Komredi Kinana kwa niaba ya wazee wa mkoa wa Lindi
0 comments:
Post a Comment