Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group,
Bw. Farough Baghozah (wapili kushoto)akimkabidhi hundi ya shilingi
milioni 13 Mratibu wa Mbio za Rock City Marathon 2014, Bw. Mathew Kasonta (wa
kwanza kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam
jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe
26 Mwezi huu. Wakishuhudia wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN
Group Bi. Pamela Mandari, na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi.
Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto).
Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw.
Farough Baghozah (wapili kulia)akifafanua jambo kwa waandishi
wa habari wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 13
iliyotolewa na kampuni hiyo kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014
zitakazofanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 Mwezi huu.
Wakishuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi. Pamela Mandari,
Mratibu wa mbio hizo, Bw. Mathew Kasonta (wapili kushoto) na Afisa Uhusiano na
Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto).
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon,
Bw. Mathew Kasonta, (wa pili kushoto) akiongea na waandishi muda mfupi kaba ya
kupokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 13 iliyotolewa na kampuni ya
TSN Group kuoitia kinywaji chake cha Chili Willy kama udhamini wa mbio hizo kwa
mwaka huu zitakazofanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26
Mwezi huu. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw. Farough
Baghozah akifuatiwa na Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi. Pamela
Mandari, na kushoto ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Koiya
Kibanga (wa kwanza kushoto).
====== ======= =========
Ukurasa
mpya umefunguliwa katika mbio za Rock City Marathon za mwaka huu ambapo kwa mara
ya kwanza tangu mbio hizo zilipoanzishwa miaka mitano iliyopita, mbio fupi sasa
zitakuwepo.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 13 kwa waratibu wa mbio
hizo kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI), Afisa Mtendaji Mkuu
wa TSN Group Bw. Farough Baghozah aliipongeza hatua hiyo, na kusema kuwa
kampuni yake inaungana na wadhamini wengine kuunga mkono tukio hilo la kila
mwaka sababu ya dhamira yake ya kuibua na kukuza vipaji vya vijana katika
riadha na kukuza utalii wa ndani kupitia michezo.
“Tunayofuraha
kuidhamini mashindano ya mwaka huu ambayo sasa yatajumuisha na vijana wadogo
ambao wana vipaji vya kukimbia mbio fupi fupi. Hii itawapa vijana wengi nafasi
ya kuonyesha vipaji vyao, ambavyo vinaweza kuwa ndiyo fani zao hapo mbeleni,”
alisema Bw. Baghozah.
Alisema
kuwa kampuni yake imekuwa ikiunga mkono jitihada mbali mbali zinazolenga kukuza
sekta ya michezo na burudani nchini Tanzania, ambayo imekuwa ikitengeneza
fursa za ajira miongoni mwa vijana walio wengi nchini.
“Hivi
karibuni tu, TSN Group iliweza kuwaleta wachezaji wa timu ya Real Madrid ili
kucheza na wachezaji wa zamani wa Tanzania wa mpira wa miguu. Hii ililenga
katika kuwatia morari wachezaji wetu na vijana kupenda michezo, wakiendelea
kuongeza jitihada ili kufanikiwa zaidi katika kile wanachofanya,” alisema.
Naye
mratibu wa tukio hilo, Bw. Mathew Kasonta alisema udhamini huo kutoka TSN Group
utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha mbio hizo za Rock City Marathon 2014,
ambapo vipaji katika mchezo wa riadha vitagundulika pamoja na kuyafanya
mashindano hayo kuwa chanzo kikubwa zaidi ya kutangaza maeneo mbali mbali ya
utalii katika kanda ya ziwa.
“Baada
ya kupata udhamini toka kwa wadhamini wetu, kamati ya maandilizi ilikaa na
kukubaliana kuwa mbio za Rock City za mwaka huu zitajumuisha mbio fupi. Hizi
zitajumuisha vijana kutoka katika shule za sekondari na wale waliopo shule za
msingi madarasa ya juu. Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kuona kuwa mashindano
ya marathon nyingi nchini, hayana mbio fupi ambazo zina vipaji vingi pia,”
alisema Kasonta.
Alisema
mbio hizo fupi zitakuwa ni; kilomita 100, kilomita 400 na kilomita 1500. Mbio
hizo zitafanyika baada ya mbio ndefu ya nusu marathoni. Bw.
Kasonta alisema fomu za usajili zinapatikana katika ofisi za kampuni ya Capital
Plus International Limited (CPI) jengo la ATC ghorofa ya tatu jijini Dar es
Salaam, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Ofisi zote za wilaya za
Michezo na Utamaduni mkoani Mwanza, Uwanja wa Nyamagana na pia zinapatikana
katika mtandao wa www.therockcitymarathon. blogspot.com.
“Meya
wa jiji la Mwanza, Bw. Stanslaus Mabula alifungua usajili kwa kuwa mshiriki wa
kwanza kujisajili katika mbio za Rock City Marathon 2014 ambazo zitaanza katika
uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu, ambapo ataonyesha uwezo
wake katika riadha kwenye mbio za kilometa 5,” alisema.
Bw.
Kasonta aliwataja wadhamini waliyofanyikisha mbio hizo kuwa ni Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy,
pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania, New Mwanza Hotel, Nyanza
Bottling, Sahara Media Group, Continental decoders, New Africa Hotel, PPF,
Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
0 comments:
Post a Comment