SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, October 9, 2014

UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC WAMKARIBISHA BALOZI OMBENI SEFUE KWA CHAKULA CHA JIONI

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwasili kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC nchini Marekani alikokaribishwa chakula cha jioni wakiwemo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania. Mhe. Ombeni Sefue ndiye aliyewezesha ununuzi wa jengo hilo la Ubalozi wakati alipokua Balozi wa Tanzania nchini Marekani mwaka 2007
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akimpokea Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue siku ya Jumatano Oct 8, 2014 siku Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipomkaribisha chakula cha jioni wakiwemo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea mawili matatu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Naibu Gavana Dr. Natu Mwamba.
Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka akiongea machche na baadae kumkaribisha Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

0 comments:

Post a Comment