Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akionyeshwa mikorosho iliyokauka katika
mashamba ya wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Magawa katika wilaya
ya Mkuranga mkoa wa Pwani, alipokagua adhari za mikorosho hiyo Sepetemba
14, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama
na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua
katika mkoa huo. Baada ya kushuhudia madhara hayo Kinana amesononeshwa
na kuahidi kulifikisha tatizo hilo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili
serikali itazame njia ya kuwafidia wakulima ili kunusuru hali za maisha
yao.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua mikorosho iliyokauka katika
mashamba ya wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Magawa katika wilaya
ya Mkuranga mkoa wa Pwani, alipokagua adhari za mikorosho hiyo Sepetemba
14, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama
na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua
katika mkoa huo. Baada ya kushuhudia madhara hayo Kinana amesononeshwa
na kuahidi kulifikisha tatizo hilo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili
serikali itazame njia ya kuwafidia wakulima ili kunusuru hali za maisha
yao.
Kinana
akisalimiana na wananchi alipowasili katika wilaya ya Rufiji, Septemba
14, 2014, wakati akiendelea na ziara yake katika mkoa wa Pwani. Kushoto
ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye ameambatana naye
katika ziara hiyo.
Kinana akimsalimia Mbunge wa rufiji alipowasilikatika wilaya hiyo
Kinana akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurudin Babu alipowasili katika wilaya hiyo, leo Septemba 14, 2014.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya
Rufiji Nurudin Babu alipowasilina Kinana katika wilaya hiyo.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Rufiji wakiwakwenye kikao chao na Kinana, wilayani humo leo, Septemba 14, 2014.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Rufiji, leo Septemba 14,2014.
Katibu
Mkuu wa CCM, Kinana, akifungua Ofisi ya mafundi seremala Mbuyuni
wilayani Rufiji, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya
Chama na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za
kuzitatua katika mkoa huo.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia Wananchi katika
mkutano wa Kinana uliofanyika katika mji mdogo wa Utete, wilayani
Rufiji, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na
kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika
mkoa huo.Nape amewataka wananchi kuendelea kuwa na Imani na CCM akisema
ndicho chama chenye uwezo wa kutatua kero zao na ndicho chenye uhakika
wa kuwa nao kwa muda mrefu kwa sababu kinaendelea kuimarika wakati vile
vya upinzani vikizidi kufa.
Katibu Mkuu wa NEC, Kinana akihutubia Wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Utete, wilayani Rufiji, akiwa
katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kusikiliza
kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa
huo.Kinana amesema, CCM itaendelea kusikiliza kero za wananchi na
kushirikiana nao kupata njia za kuzitatua katika njia iliyo sahihi.
Wanachama
wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao za uanachama na
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, katika mkutanowa hadhara
uliofanyika leo, Septemba 14, 2014 katika mji mdogo wa Utete, wilayani
Rufiji mkoa wa Pwani. Jumla ya wanachama wapya 180 walipewa kadi. Picha
zote na Bashir Nkoromo.
0 comments:
Post a Comment