Naibu
Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya
Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Humphrey Mniachi akiongea na waandishi
wa Habari (Hawapo Pichani)Jinsi wanavyoshirikiana na Vyombo vingine
serikalini katika Mchakato wa Ajira,wakati wa Mkutano uliofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi
Hiyo Bi. Riziki Abraham.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira
katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham akieleza kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu mambo ya kuzingatia kabla ya kuomba kazi
nchini kwa waombaji waliopotelea na vyeti, kuibiwa vyeti au kubadilisha
majina,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni
Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi hiyo Bw.Humphrey
Mniachi.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka Ofisi ya
Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Jijini Dar es
Salaam.(Picha na Hassan Silayo)(Martha Magessa)
Na Georgina Misama
Serikali
imewataka waombaji kazi waliobadilisha majina, waliosoma nje ya Nchi,
kupoteza, kuibiwa, kuharibikiwa au kuunguliwa na vyeti kufuata taratibu
pindi wanapoomba kazi secretariati ya ajira.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Rais,
Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham wakati
wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Riziki
alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko toka kwa waombaji wa kazi
kuwa secretariati ya Ajira imekuwa na upedeleo kwa kutowaita au
kuwazuia kufanya usaili waombaji wasiokuwa na nyaraka halisi.
Riziki
alifafanua kuwa pindi waombaji wanapokabiliwa na hali hiyo hawana budi
kutoa tarifaa katika mamlaka husika ili taratibu za kupata vyeti vingine
zifanyike na taarifa zao kutumwa Secretariati ya Ajira kwa wakati.
Akizitaja
Mamlaka hizo Riziki alisema ni Polisi, Baraza la Mitihani la Taifa
(NECTA), Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Tume ya Vikuu (TCU),
na Baraza la Usimamizi wa Elimu ya Vyuo vya Ufundi (NACTE).
Aidha,
Riziki aliongeza kuwa kwa waombaji wenye majina tofauti kwenye vyeti
wanapaswa kwenda mahakamani na kula kiapo kwa kamishna wa viapo au kwa
wakili ili waweze kupata (Deedpal) au (Affidavity) kwa mujibu wa sheria
na kwakufanya hivyo itasaidia kuthibitisha uhalali wa tofauti ya majina
na kutambulika kisheria.
Sekretarieti
ya Ajira inapenda kuwafahamisha wadau wake, hususani waombaji kazi
Serikalini kwamba haipokei barua ya utambulisho kutoka polisi inayohusu
kupoteza, kuungua, kuibiwa, utofauti wa majina kati ya cheti kimoja na
kingine kutokana na baadhi yao kuzitumia vibaya.
0 comments:
Post a Comment