Mabingwa watetezi wa kombe la
dunia Uhispania wameambulia kichapo cha mabao 5-1 mikononi mwa timu
walioishinda katika fainali ya kombe la dunia huko Afrika Kusini miaka
minne iliyopita.
Kabla ya leo Uhispania ilikuwa haijashindwa katika dakika 476 ya mechi za kombe la dunia.
Mabao hayo ni zaidi ya mabao yote waliofungwa katika mchuano wa Euro na kombe la dunia la mwaka wa 2010 huko Afrika Kusini.
Uholanzi ilitoka nyuma baada ya Xavi Alonso kuiweka Uhispania mbele kwa mkwaju wa penalti baada ya Diego Costa kuangushwa katika eneo la hatari.
Hata hivyo Robin van Persie aliisawazishia Uholanzi kwa mkwaju wa kipekee wa kichwa dakika moja tu kabla kipindi cha kwanza hakijakamilika.
Mabingwa hao wa dunia hawakuwa na majibu ya wimbi baada ya wimbi ya mashambulizi kutoka Uholanzi Arjen Robben Robin van Persie na Wesley Sneijder waliposhirikiana kwa karibu na juhudi zao zikazaa matunda .
Arjen Robben aliiweka Uholanzi mbele kunako dakika ya 53.
Hata hivyo masihara ya kipa Iker Cassillas yalipelekea RVP kufunga bao lake la pili na hivyo kumhakikishia kocha Van gal alama tatu muhimu katika mechi yao ya kwanza ya kundi lao.
Robben kwa upande wake aliidhalilisha safu ya ulinzi ya Uhispania na kufuma bao lake la pili na la tano kwa kocha Van Gaal.
Kufuatia kichapo hicho Mabingwa hao watetezi walishuka hadi nafasi ya mwisho kwenye kundi B wakiwa wametinga idadi kubwa ya mabao ikilinganishwa na Australia na Chile .
SIKU YA JANA PIA MECHI KATI YA MEXICO NA CAMEROON
Mexico yailaza Cameroon bao 1-0.
Mexico yajikita katika nafasi ya
pili ya Kundi A nyuma ya Brazil baada ya ushindi wa bao moja kwa nunge
dhidi ya wawakilishi wa Afrika the Indomitable lions ya Cameroon.
Mechi hiyo ndiyo iliyokuwa ya pili baada ya ushindi tata wa Brazil dhidi ya Craotia hapo jana.Kama mechi hiyo ya ufunguzi iliyoshuhudia maamuzi tata, Mabao mawili ya mshambulizi wa Giovanni Dos Santos yalifutiliwa mbali kutokana na kile wachambuzi wa mechi waliashiria kuwa ni makosa ya naibu wa refarii.
Licha ya hayo Mkwaju wa Dos Santos ulipanguliwa na kipa wa Cameroon kabla ya Oribe Peralta kufuma bao hilo la pekee na la ushindi kunako dakika ya 61 ya kipindi cha pili.
Mexico sasa inatoshana nguvu na Brazil kileleni mwa kundi A.
20:55 Mechi imekamilika Mexico 1-0 Cameroon
20:53 Hernandes anapoteza nafasi ya wazi ya kuongeza bao la pili la Mexico.
20:53 Dakika nne za ziada Mexico 1-0 Cameroon
20:44 Matokeo bado ni Mexico 1-0 Cameroon dakika ni ya 82
20:42 Mexico wanashambulia lango la Cameroon zikiwa zimesalia dakika 8 tu ya mechi hii ya Kundi A
20:41 Mkwaju unapigwa na kupanguliwa mara moja na Mexico,inakuwa Goal Kick.
20:41 Samuel Etooooo ah ! ,,,Kona kuelekea lango la Mexico.
20:40 Badiliko la Cameroon A. Song aondoka na nafasi yake inatwaliwa na WeBo.
20:39 Matokeo bado ni Mexico 1-0 Cameroon dakika ni ya 78
20:38 Free Kick kuelekea lango la Cameroon
20:35 Kufikia sasa Mexico wametawala mechi hii kwa asilimia 65 % huku Cameroon wakicheza asilimia 35 %
20:32 Javier Hernandez anachukua nafasi ya mfungaji bao la Mexico Oribe Peralta
20:31 Mabao bado ni Mexico 1-0 Cameroon Kunako dakika ya 70 ya kipindi cha pili
20:29 Mexico wafanya badiliko la kwanza Andres naondoka Marco anachukua nafasi yake uwanjani .
20:21 BAOOOOOO Mexico 1-0 Cameroon
20:20 Na sasa Mexico wanajibu Mashambulizi 'First Break ya Mexico.
20:19 Mkwaju wa Freekick unagonga ukuta na sasa ni Kona.
20:17 Hector Moreno anaoneshwa kadi ya njano kwa kumwangusha Etoo.
20:16 Uwanja umelowa maji lakini Samuel Ettoo anajaribu kukwepa safu ya ulinzi ya Mexico.
20:16 Mabao bado ni Mexico 0-0 Cameroon
20:15 Tupe maoni yako kwenye facebook tafuta BBCSwahili na utuwachie ujumbe wako.
20:15 Je mabao ya Giovani yaliyokataliwa yalikuwa halali ?
20:13 Cameroon wafanya shambulizi lao la kwanza katika kipindi cha pili katika lango la Mexico lakini mkwaju ni hafifu mno .
20:11 Dos Santos bado amelala chini refarii anapeana mkwaju wa adhabu.
20:10 Dos Santos ni mwiba katika safu ya ulinzi ya the Indomitable Lions
20:08 Cameroon yanusurika hapa. dakika mbili tu baada ya kipindi hichi cha pili kuanza.
20:08 Matokeo bado ni Mexico 0-0 Cameroon
20:07 Kipindi cha pili kinaanza hapa.
20:06 Mexico walitawala kipindi cha kwanza cha mechi hii ya kwanza inayohusisha timu kutoka Afrika
20:04 Refarii waendelea kuibua hisia kali kutokana mamuzi yao uwanjani.
Vijana wa Cameroon dhidi ya Mexico.
Una fursa ya kutupa utabiri wako kuhusu timu unayodhani itashinda mchuano wa leo kupitia kwenye ukurasa wetu wa Facebook..Bofya https://www.facebook.com/pages/BBC-Swahili/160894643929209
Emmanuel Kunzugala unasema kupitia ukurasa wetu wa Facebook : Cameroon itaibuka mshindi Lakin kwa Mexico wakae chonjo
19:10 PM: Kona kwa upande wa Cameroon ila mpira umepigwa nje tena
19:17 PM: Mexico imeingiza bao ingawa refari amepuliza kipenga kusema kuwa bao lilikuwa Offside.
19:15 PM: Baada ya dakika kumi na moja na seekunde kumi na moja mchezo bado ni sare ya bila bila.
HABARI NA BBC SWAHILI