Mtu mmoja ameripotiwa kufariki huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika shambulizi la bomu kisiwani Zanzibar.
Baadhi ya waathiriwa walikuwa wanaondoka katika msikiti mmoja ulioko katika mji mkuu wa Stone Town.
Ni
shambulizi la pili la bomu mwaka huu.Haijulikani ni nani aliyetekeleza
shambulizi hilo ambalo linajiri mkesha wa sherehe za kimataifa za filamu
katika kisiwa hicho.
Mnamo
mwezi February, mabomu mawili tofauti ya kujitengezea yalilipuliwa nje
ya kanisa Anglikana mjini Stone Town pamoja na mkahawa uliokuwa karibu
na kanisa hilo.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi wa kidini katika kisiwa hicho.
SUFIANI MAFOTO