Kazi ya kuzima moto ikiendelea.
Jitihada za kuuzima moto huo bado zinaendelea.
Moto bado unaendelea kuwaka mpaka wakati huu,huku jitihada mbali mbali za kuuzima moto huo zikiendelea.
Baadhi
ya wafanyabiashara na mashuhuda wa tukio hilo wakiangalia huku wakiwa
hawajua la kufanya,maana mali zote zimeteketea kwa moto huo.
Soko loote limeteketea kwa moto huo.
Sehemu
ya wafanya Biashara wa soko hilo,wakimuangalia mmoja wa wamachinga
akipanga nguo kwenye kibanda chake alichokuja nacho huku wenzie
wakiendelea kusikilizia machungu ya kuunguliwa na mali zao.
Mijadala ya hapa na pale huku moto ukiendelea kuwaka. Sehemu
ya wafanyakazi wa Kikosi zimamoto wakiendelea na zoezi la kuzima moto
ulioteketeza kabisa Soko la Ilala Mchikichini Jijini Dar es salaam
leo.Moto huo ulianza majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo na
kuteketeza kila kilichokuwepo katika eneo la soko hilo. Chanzo cha
kutokea kwa moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa.
Picha zote na Othman Michuzi.
Picha zote na Othman Michuzi.