Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha jana. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka. (Na Mpiga Picha Wetu)
Washiriki wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika Semina hiyo.
Washiriki wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika Semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika semina iliyofanyika jijini Arusha leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi, Martin Mmari wakati wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB jijini Arusha leo.
Mmoja wa wanahisa akichangia mada.
Mshiriki wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Kamanga Khamis kutoka Mkoa wa Kilimanjaro akizungumza wakati wa Semina hiyo iliyofanyika jijini Arusha.
Wanahisa wakifuatilia mada.
Mshiriki wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Kamanga Khamis kutoka Mkoa wa Kilimanjaro akizungumza wakati wa Semina hiyo iliyofanyika jijini Arusha.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
Mshauri wa Masuala ya Fedha, Prof. Mohamed Warsame akitoa mada wakati wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Arusha.
Wanahisa wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa semina.
Mshauri wa Masuala ya Fedha, Prof. Mohamed Warsame akitoa mada wakati wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafitio na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akiwa katika semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB.
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye (kushoto), ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB akiwa katika semina ya Wanahisa wa CRDB. Katikati ni Mshauri wa Masuala ya Fedha, Prof. Mohamed Warsame
Benki ya CRDB inatarajia kuuza Hisa zake katika Soko la Hisa la Nairobi, fursa ambayo itatoa wigo mpana zaidi wa biashara ya hisa za Benki hiyo katika soko la Afrika Mashariki.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakati wa siku ya kwanza ya mkutano mkuu wa wanachama wote unaofanyika hapa jijini Arusha.
Kimei alisema uuzaji wa hisa katika Soko la Hisa la Nairobi utafanya bei ya hisa za benki ya CRDB kupanda kutokana na ukweli kwamba katika soko la Dar es Salaam bei ya hisa zote ipo chini sana.
Mfano kama ingeweza kufanyika mahesabu ya kitaalam, bei halisi ya hisa ya CRDB ingetakiwa iwe zaidi ya shilingi 500 badala ya 310 ya sasa. Na kitendo cha kuuza hisa kwenye soko la Nairobi ina maana wafanyabiashara wengi watavutiwa na wataweza kununua na kuuza hisa hizo.
Pia ikizingatiwa ukweli kuwa sehemu kubwa ya wanahisa wa Benki ya CRDB ni wanahisa mmoja mmoja ambao huuza na kununua hisa zao kutokana na hali ya maisha inayowakabili kwa wakati Fulani.
Kumbe kwa kuingia kwenye Soko la Nairobi ina maana kutakuwa na mchanganyiko na wafanyabiashara wakubwa.