Meneja
wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael (kulia)
akimkambidhi mfano wa hundi cha kiasi cha Tsh 20,700,000 Kaimu Katibu
Mkuu wa Shirika la Red Cross nchini Bi. Bertha Mlay mapema leo katika
hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika makao makuu ya Red Cross,
jijini Dar es Salaam. Kiasi hicho kinalenga kuwapatia waathirika wa
mafuriko wa Dumila – Morogoro na Dar es Salaam huduma za malazi, maji,
chakula, mablanketi, neti za kuzuia mbu na magodoro.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Shirika la Red Cross nchini Bi. Bertha Mlay (katikati)
akipokea kwa furaha moja ya mifuko ya sembe kutoka kwa Meneja wa Huduma
kwa Wateja wa Tigo Bi. Halima Kasoro mapema jana. Wafanyakazi wa Tigo
waliweza pia kujichanga kiasi cha Tsh 4,000,000 ambayo imesaidia kununua
vyakula hivyo.
Baadhi
ya vyakula vilivyotolewa kama msaada na wafanyakazi wa kampuni ya simu
ya Tigo kwa waathirika wa mafuriko wa Dumila – Morogoro na jiji la Dar
es Salaam.
Meneja
wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano wa msaada wa
fedha na vyakula kwenda kwa waathirika wa mafuriko nchini. Zaidi ya
familia 800 zitanufaika na msaada huu, familia 400 kutoka Dumila –
Morogoro na 400 wengine kutoka jijini Dar es Salaam. Bi. Shisael pia
alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali pamoja na Shirika la Red Cross
Tanzania kwa jitihada zao mpaka sasa.
Wafanyakazi wa Tigo katika picha ya pamoja nje ya jengo la Shirika la Red Cross Tanzania, jijini Dar es Salaam.