Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu ukaguzi maalum wa
maduka ya kuuzia vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika
jiji la Dar es salaam kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na Vipodozi
sura ya 219.
Mkurugenzi
wa Usalama na Chakula wa TFDA Bw. Raymond Wigenge akitoa ufafanuzi kwa
waandishi kuhusu hatua zinazochukuliwa na TFDA kuhakikisha usalama wa
vyakula na Dawa nchini .TFDA imekuwa ikiongeza nguvu katika kukabiliana
na bidhaa zisizokidhi viwango kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za
udhibiti kwa kukagua, kukamata na kuchukua hatua za kisheria ikiwemo
kuwafikisha mahakamani wanaokiuka sheria.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo (kulia) akitoa
ufafanuzi wa baadhi ya bidhaa zilizokamatwa katika ukaguzi maalum kwenye
maduka ya kuuzia vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika
jiji la Dar es salaam zikiuzwa kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na
Vipodozi sura ya 219. Wengine ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa
TFDA Bw. Raymond Wigenge, na Meneja wa Ukaguzi wa Chakula wa TFDA kanda
ya Mashariki Bw. Emmanuel Alphonce.
Afisa
Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) akiwaonesha waandishi wa
habari baadhi ya bidhaa zilizokamatwa na mamlaka hiyo zikiwemo chumvi,
vinywaji, maziwa ya watoto ambazo hazijasajiliwa na mamlaka hiyo
kufuatia ukaguzi maalum uliofanyika katika jiji la Dar es salaam.
Maziwa
ya watoto aina ya SMA 1,2 na 3, Promil Gold, S-26 Gold, Nursoy,
Progress Gold, Cow & Gate, Isomil 2 na Infacare Soya , Nutrikids na
Aptimil 1 yaliyokamatwa ambayo hayajasajiliwa na TFDA .
Vinywaji
baridi ambavyo havikusajiliwa na TFDA vilivyokamatwa kufuatia ukaguzi
maalum katika jiji la Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa.