SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 4, 2014

Shule ya Motamburu Moshi yapata msaada wa vitabu toka Airtel.

 Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwanafunzi Happnes John wa shule ya sekondari motamburu moja ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu kwa shule ya sekondari Motamburu iliyopo Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwalimu mkuu(Abel Masuki kushoto) wa shule ya sekondari motamburu baadhi ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu shuleni hapo
======  ====== =======
Shule ya Motamburu Moshi yapata msaada wa vitabu toka Airtel.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Program yake ya  shule yetu  imeendelea na zoezi lake la kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo  ya sayansi ambapo imekabidhi vitabu vya ziada na kiada katika masomo ya sayansi  kwa shule ya  sekondari ya MOTAMBURU   iliyopo  Kata ya tarakea  wilaya ya  Rombo mkoani Kilimanjaro.

Akizungumzia msaada huo  Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala   alisema" program ya shule yetu inayolenga kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni  ikiwemo  vitabu vya kiada na ziada   kwa upande wa masomo ya sayansi  ambapo mpaka sasa wameweza kufikia shule 900 katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na visiwani ".

"Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha elimu mashuleni na kupunguza changamoto za upatikanaji wa vitabu katika shule nyingi nchini. sliongeza Majwala

Mkuu wa wilaya ya Rombo Elinasi Pallangyo  ambaye ndio  alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi za makabidhiano hayo ,alipokea msaada wa vitabu  na kuukabidhi  kwa uongozi wa shule baada ya kukabidhiwa na meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini ambapo amewashukuru airtel kwa msaada huo ambao amesema  umekuja wakati muafaka  huku akiwakumbusha wadau wengine kuiga mfano wa Airtell Katika kuchangia maswala muhimu ndani ya sekta ya elimu hususani katika maeneo ya vijijini.

Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya shule kwa mkuu wa wilaya  mkuu wa shule ya  sekondari MOTAMBURU Abel Masuki  ameishukuru airtel Tanzania kwa msaada huo ambao wamesema Airtel imeonyesha kuwa mfano mkubwa kwa makampuni mengi kwa kuungana na serikali kutekeleza sera  ya  elimu ya kuwaelimisha watanzania wengi  hasa walio  maskini kuwaondolea ujinga lakini pia akatoa changamoto ya vifaa vya maabara.