Katibu Mwenezi wa Chaso Iringa, Michael Noel akizungumza kushoto kwake ni mwenyekiti wa chaso mkoa wa Iringa Thimotheo Mkanyia.
baadhi ya viongozi wa chaso kutoka katika vyuo vikuu vilivyoko mkoa wa Iringa wakiwa katika ofisi za chama hicho.
======== ======== ========
CHASO IRINGA WATOA TAMKO KUHUSU RASIMU YA KATIBA MPYA
Na Denis Mlowe.
JUMUIYA
ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Wanachadema Mkoa wa Iringa (CHASO)
wamelaani vikali mwenendo mbovu wa Bunge Maalum la Katiba katika
kuendesha na kujadili rasimu ya katiba tangu lilipoanza kwa kuendesha
malumbano kila kwenye kikao na wakati mwingine wajumbe kuzomeana na
kuacha kujadili mambo ya msingi yanayowagharimu Watanzania mamilioni ya
Fedha.
Wakitoa
msimamo mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Chaso zilizoko
Tumaini katika kata ya Kihesa jana, Katibu Mwenezi wa Chaso Iringa,
Michael Noel alisema bunge la katiba limepoteza imani kwa wananchi na
wamekuwa wakilipwa posho kwa kodi zetu, wanataka watupatie katiba ya
msimamo wa chama cha mapinduzi.
Alisema
kuwa chaso haiko tayari kuona mawazo ya wananchi katika rasimu ya
katiba yanapotoshwa kwa misingi ya faida ya chama kimoja hivyo wako
tayari kuandamana nchini nzima endapo ccm watapitisha katiba yenye
msingi ya maslahi ya chama chao.
Alifafanua
kuwa wajumbe wa vyama vya siasa vya upinzani wamekuwa wakibaguliwa na
wakati mwingine kutosikilizwa hoja zao hata kama za msingi kwa kuwa
hawafungamani na chama cha mapinduzi.
“ Hata
wenyeviti wa kamati nyingi za bunge hilo ni wa ccm kitu kinachowasaidia
kuchakachua kanuni ili kuwarahisishia kutekeleza dhamira yao ya
kubadilisha vifungu vya rasimu hasa mfumo wa muungano ambao
umependekezwa na tume kupitia maoni ya wananchi” alisema Noel
Aliongeza
kuwa kuna tuhuma za rushwa zinazosikika kila kukicha lakini hakuna
hatua zozote zinazochukuliwa kwa wajumbe wanaotuhumiwa na tuhuma zote
hizi ni dhidi ya wajumbe wa ccm wakiwamo mawaziri wa serikali na kuhoji
wanafanya hivyo kwa dhamira ipi?
Noel
alisema wajumbe wa bunge hilo wanatakiwa kutambua kuwa waamuzi wa mwisho
ni wananchi hivyo ccm isitumie hila kuwachagulia katiba waitakayo kwa
maslahi ya chama hicho na kuongeza watahamasisha wananchi popote walipo
waikatae kama rasimu hiyo itachakachuliwa na kubeba msimamo wa ccm
uliotangazwa na katibu mwenezi Nape Nnauye.
Alisisitiza
kuwa maoni ya wananchi yazingatiwe na hawako tayari kuona chama tawala
wakipuuza na kujiona wao wana hisa juu ya mfumo wanaoutaka.
“Chama
cha Mapinduzi kisijidanganye kuwa mchakato huu wakiuvuruga tutaendelea
kuitumia katiba iliyopo iliyosababisha taifa makovu makubwa
yanayoendelea kututafuna bali watasababisha taifa kuingia katika
machafuko ambayo kama busara ikitumika tunaamini katiba mpya itapatikana
kwa utulivu na amani.” Alisema Noel
Alisema
msimamo wa chaso kuunga mkono mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu ya
katiba ambayo maoni yake yametolewa na wananchi walio wengi.
Aidha
Noel amesema wamesikitishwa na hotuba aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete
wakati akifungua bunge maalum kwa kuendeleza msimamo wa ccm kwa kutaka
mawaziri watokane na wabunge.
Akifafanua
alisema hotuba ya Kikwete ni kupigiria msimamo wa ccm na kukejeli maoni
ya wananchi ambao ndio waliomuweka madarakani kunaashiria usaliti
mkubwa kwa wananchi walioamua namna mfumo mzuri wa kuendesha nchi.
“Itambulike
kuwa serikali iliyopo madarakani ni ya CCM lakini Tanzania na maisha ya
watu wake siyo mali ya CCM, hivyo kitendo cha kuwalazimisha wananchi
juu ya hatima ya nchi yao kinachofanywa na CCM hakikubaliki. Kama
tunataka katiba bora lazima ibebe maoni na matarajio ya wananchi na ndio
maana tuanaza na maneno ‘Sisi wananchi’ na sasa kama CCM haikubaliani
na maoni ya wananchi maana yake katiba ianze na maneno ‘Sisi CCM’ kitu
ambacho hakikubaliki” alisema Noel
Noel
alisema kazi ya bunge maalum la katiba siyo kubadilisha bali ni
kuboresha kwamba mambo gani yanapaswa kuingizwa ama kutolewa ndani ya
mfumo wenyewe na kutolea mfano mambo ya muungano na yasiyo ya muungano
na vyanzo vya mapato.