Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi
na Mabalozi wastaafu kwa mujibu wa sheria.
3.
Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemteua Ndugu Joseph Edward Sokoine
kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kabla ya uteuzi huu,
Bw. Sokoine alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Mkuu wa Utawala katika
Ubalozi wa Tanzania, Ottawa, Canada.
Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:
1.
Balozi Dora Mmari Msechu ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Stockholm, Sweden. Hadi uteuzi huu unafanyika
Balozi Dora Mmari Msechu ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Anachukua
nafasi ya Balozi Mohamed M .H. Mzale ambaye amestaafu.
2.
Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba, ameteuliwa kuwa Balozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moscow, Urusi. Hadi uteuzi huu
unafanyika, Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba alikuwa Mkuu wa Utendaji
Kivita na Mafunzo, Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Anachukua nafasi ya Balozi Jaka Mwambi.
Umetolewa na:
(John M. Haule)
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE
NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.