SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, April 17, 2014

Makamu wa Rais Dkt. Bilal afungua kongamano la mradi wa maisha, unaohusu afya ya mama na mtoto, Jijini Dar

01

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kupata maelezo kutoka kwa Meja Ali Kitundu, kuhusu elimu ya awali kwa wanafunzi wanaojifunza elimu ya afya kabla ya ajira, wakati alipofika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufungua Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto.  Kutoka kulia ni Dkt. Grace Qoro, Waratibu wa mradi huo, Jasmine Chechewa na Shallah Ukende. (Picha na OMR).


02

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi ya kumhudumia mama mjamzito kutoka kwa Mratibu Msaidizi wa Afya Mzazi na Mtoto wa Wilaya ya Ilala, Edith Mboga, wakati alipofika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufungua Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto.  Kulia ni Mshauri wa Ukunga Mradi wa Maisha, Scholastica Chibehe.

04

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia, wakati alipofika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufungua Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto.

05

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti mwakilishi wa Mradi wa Maisha kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto, jijini Dar es Salaam.

06

06

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti mwakilishi wa Mradi wa Maisha kutoka Mkoa wa Morogoro, ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Eliya Ntandu,  wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto, jijini Dar es Salaam.

07

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti mwakilishi wa Mradi wa Maisha Rasi wa  Mkoa wa Singida, Liana Hassan,  wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto, jijini Dar es Salaam.

08

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waratibu wa Kongamano hilo baada ya ufunguzi rasmi leo jijini Dar es Salaam. (Picha na OMR).