SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, March 4, 2014

VITUKO NA MATUKIO ULIYOKOSA KATIKA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHONI 2014

Mbio pekee inayochukua wakimbiaji wengi zaidi ni Vodacom 5km fun run na safari hii mbio hizi zilianzia jirani kabisa na Zumba .
Wadada wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,MUWSA pia walikuwepo katika mbioz hizo.
Wenye ulemavu pia walishiriki vyema kabisa.
Hatimaye wakahitimisha mbio katika uwanja wa Ushirika.
Kuna wakimbiaji wengine walitiliwa shaka kama ni washiriki ama walaikuwa na kazi nyingine kama huyu aliyekuwa akihitimisha mbio za Km 42 bila ya kuwa na namba ya ushiriki.
Huyu nae alihitimisha mbio kwa kuchechemea.
Mshiriki huyu sasa yeye alikuwa anahitimisha mbio za Km 21 akiwa amebeba mfuko uliokuwa na vitambaa vya kufunga kichwani ,swali je alikimbia huku akiendelea na biashara kwa wakimbiaji?
Hapa sasa,huyu jamaa alilzimika kuhitimisha mbio akiwa peke yake maana kila mkimbiaji aliyemsogelea alionekna kutokuwa na imani nae.
Huyu alichomoka Tuition akaamua na yeye kuhitimisha mbio akiwa na madaftari yake.
Wazee wa viatu vya matairi pia walikuwepo kutoa burudani.
Baada ya kujaa upepo kwa muda mrefu Puto hili lianza kuanguka taratibu ili kutoa nafasi kwa wapiga picha waweze kupiga kilele cha mlima Kilimanjaro kwa ufasaha.
Hatimaye likatoa shughuli nyingine kwa watu waliokuwa na kazi ya kurekodi wakimbiaji.
Wakimbiaji walihitimisha mbio kwa kuinama.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.

0 comments:

Post a Comment