Sehemu ya Magomeni jijini Dar es salaam ikonesha maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo
Kituo cha Magomeni Kagera
Daraja la Manzese pamebadilika
Daraja la waendao kwa miguu stendi ya mabasi ya bara ya Ubungo
Flyover ya waendao kwa miguu Ubungo
Kampuni ya Strabag International
GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi
Kivukoni jijini Dar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa inakamilisha
ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba
wao unavyoelekeza.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa
agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa
ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es
Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit - BRT) ambao umeelezewa kuwa na
changamoto nyingi kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumia barabara
hiyo kwa kipindi kirefu.
Akimpatia taarifa ya utekelezaji wa
mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha
Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwakazi na
mradi unaendelea kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna
ucheleweshaji zaidi katika hatua hii iliyobaki.
Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi
pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa
umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya
Shilingi bilioni 280.
CHANZO:MTAA KWA MTAA
0 comments:
Post a Comment