SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, March 6, 2014

BREAKING NEWS:- MZUNGU TAPELI ANASWA NA MAHERA KIBAO FEKI HAPA BONGO ONA HABARI YAKE YA KWANZA LIVE!!

 
Kamanda Suleiman Kova
 JAN ELOFF AKITOLEWA  NJE YA
KITUO CHA POLISI OYSTERBAY KWA AJILI KUTAMBULIWA NA MWANAHABARI WETU
JAN ELOFF AKIHOJIWA NDANI YA CHUMBA MAALUM KILICHOPO NDANI YA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY
  
Hapa akitia huruma
 
Yule mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae amekamtwa kikomandoo akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki.
Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa South Africa aliyefahamika kwa jina la  JAN ELOFF ambae anaishi maeneo ya Msasani Jijini Dar.
Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na mtandao huu hatari kwa habari za uchunguzi zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi (jina kapuni) na DTV Bw. Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU,pamoja na Kutoa Euro Feki.
Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni raia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukamatwa mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana nao.
Kufuatia kukamtwa kwa mzungu huyo wananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha kukamatwa mzungu huyo. Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi kupigwa na mzungu huyo basi wafike haraka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo.

0 comments:

Post a Comment