Mkuu
wa Tawi la Uchunguzi wa Kesi, katika Jimbo la Kwa Zulu-Natal, Brigedia
Clifford Marion, alisema Stephen Ongolo ambaye ni raia wa Tanzania
anayekabiliwa na madai ya kutishia kutoa siri za mke wa Rais Jacob Zuma,
Nompumelelo Ntuli (MaNtuli), huenda akarudishwa nchini na kuzuiwa
kuitembelea Afrika Kusini milele.
Akiongea wakati wa kusikilizwa kesi hiyo katika Mahakama ya Camperdown, jijini Durban, Brigedia
Marion alisema “Ongolo si raia wa Afrika Kusini na Viza yake
inamalizika Februari 18 mwaka huu na atarudishwa nchini mwake Tanzania
na hatarudi tena Afrika Kusini,” alisema Marion.
Kuhusiana na tuhuma dhidi ya Stephen Ongolo,
Brigedia Marion alitoa ushahidi kuwa Ongolo amekuwa akituma ujumbe mfupi
kwenye simu ya MaNtuli, akimtishia kuwa atatoa siri kuhusu uhalali wa
mtoto wake (MaNtuli).
Inadaiwa kuwa Ongolo katika ujumbe wake alidai kuwa mtoto mmoja wa MaNtuli si wa Rais Zuma.
Kabla
ya kukamatwa, Ongolo alikwenda katika vyombo vya habari kadhaa vya
nchini humo na kudai kuwa, anafahamu siri nzito kati ya MaNtuli na
Phinda Thomo, aliyekuwa mlinzi wa MaNtuli.
Thomo, alikutwa
amejiua mwaka 2009 bafuni kwake, lakini Ongolo anadai kuwa Thomo
hakuuawa na badala yake, kifo chake kilipangwa kutokana na uhusiano wa
siri kati yake na MaNtuli.
CREDIT..DAR 24
0 comments:
Post a Comment