SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, February 2, 2014

Mapokezi ya Rais wa Zanzibar Nchini India


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake wakiongozana na Balozi wa Tanzania Nchini India John W.H.Kijazi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indra Gandhi,Rais atakua nchini India kwa ziara rasmi ya siku tisa.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na akizungumza na Balozi wa India nchini Tanzania Debnath Shaw katika ukumbi wa VIP wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indra Gandhi Nchini India Rais akiwa huko atatembelea sehemu mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana Wanawake na Watoto,Bi Zainab Omar,wakiwa katika ukumbi wa VIP wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indra Gandhi Nchini India Ujumbe wa Rais Dk.Shein, utatembelea sehemu mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.


Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim,ni miongozi mwa ujumbe wa Rais wa Zanzibar katika safari rasmi nchini india,hapa wakiwa katika ukumbi wa VIP wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Indra Gandhi Nchini India ambapo utatembelea sehemu mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wa walikaribishwa kwa ngoma za asili mara baada ya kufika katika hoteli ya Oberoi Taj Vilas,katika jimbo la Rajastani Nchini India Rais akiwa huko atatembelea sehemu mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe aliofuatana nao wakipata maelezo kutoka kwa Kiongozi Panraj Dharendra,katika Sehemu ya Historia inayoitwa Amber,wakati alipotembelea sehemu hiyo maarufu katikan jimbo la Rajastan Nchini India,akiwa huko Rais atatembelea Taasisi mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha wageni wanaotembela Sehemu ya Historia inayoitwa Amber, maarufu katika jimbo la Rajastan Nchini India,RAIS akiwa huko atatembelea Taasisi mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembela Sehemu ya Historia inayoitwa Amber, maarufu katika jimbo la Rajastan Nchini India,RAIS akiwa huko atatembelea Taasisi mbali mbali ikiwa ni katika kukuza Uhusiano na mashirikiano ya kiuchumi na Kijamii.
Picha na Ramadhan Othman,India 



0 comments:

Post a Comment