Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Balozi mpya wa Oman nchini Tanzania, Soud Ali Mohamed Al
Ruqaishi, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo Feb 7, 2014 kwa mazungumzo, alipofika kujitambulisha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Balozi mpya wa Oman nchini Tanzania, Soud Ali Mohamed Al
Ruqaishi, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Makamu Ikulu
jijini Dar es Salaam, leo.
---
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amempokea Balozi mpya wa Oman
nchini Tanzania Balozi Soud Ali Mohamed Al Ruqaishi ofisini kwake Ikulu
Jijini Dar es Salaam na kisha kufanya naye mazungumzo. Katika mazungumzo
hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais amemhakikishia Balozi Ruqaishi kuwa
Tanzania na Oman zina uhusiano wa kindugu wa siku nyingi na kwamba
uhusiano huo umekuwa ukinufaisha nchi hizi kwa miaka kadhaa.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais aliendelea kufafanua kuwa, Tanzania kwa sasa
inashirikiana na Oman kiuchumi na kwamba kuna wawekezaji wengi kutoka
Oman ambao wako nchini, sambamba na wengine wanaoonesha nia ya kuwekeza
katika sekta mbalimbali hapa Tanzania.
Kwa
upande wake Balozi Ruqaishi alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa,
Oman inafurahia uhusiano wake na Tanzania na kwamba jukumu lake la
kwanza ni kuhakikisha kuwa uhusiano huo unadumu na kunufaisha nchi hizi
mbili. Pili alifafanua kuwa, atahakikisha katika kipindi chake cha
Ubalozi hapa Tanzania anasaidia kutanua fursa za uwekezaji kwa
wawekezaji kutoka Oman sambamba na kuwafungulia fursa kama hizo
wawekezaji walio na nia ya kuwekeza nchini Tanzania.
Oman
licha ya kuwa na uhusiano wa karibu na Tanzania na hasa Visiwani
Zanzibar, inabakia kuwa ndiyo nchi pekee duniani nje ya Afrika iliyo na
wazungumzaji wengi wa lugha ya Kiswahili. Katika siku za hivi karibuni,
wawekezaji kutoka Oman wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya Mafuta
na Gesi sambamba na kuliimarisha shirika la Ndege Tanzania ili limudu
ushindani na kuongeza ufanisi wa shughuli zake katika biashara ya safari
za anga.
Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam,
Ijumaa Februari 07, 2014
0 comments:
Post a Comment