Katibu Mkuu wa Chadema, Willibrod Slaa na mwenyekiti wake Freeman Mbowe
wakielekea kuzungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya chama
hicho Dar es Salaam jana kuhusu kuanza kwa ‘Operesheni Pamoja Daima’ ya
kuzunguka nchi nzima ili kuimarisha chama hicho. Picha na Fidelis
Felix
----
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuanzia leo,
kinarusha helkopta tatu kwa siku 14 mfululizo, katika kutekeleza
kampeni iliyopewa jina la Operesheni Pamoja Daima (ODB) itakayoendeshwa
katika mikoa yote nchini.
Ziara hiyo inaanzia katika mikoa ya Tanga, Mwanza
na Ruvuma, huku viongozi wa chama hicho wakijigawa katika makundi sita;
matatu yakitumia helkopta na matatu yatawafikia wananchi kwa kutumia
usafiri wa magari.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema jana
jijini Dar es Salaam kuwa, lengo la operesheni hiyo ni kukiimarisha
chama hicho na kuwafumbua macho wananchi kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.
“Tumejigawa katika makundi sita na makundi matatu
kati ya hayo yatatumia helikopta kila moja, makundi mengine yatawafikia
wananchi kwa misafara ya ardhini,” alisema Mbowe na kuongeza;
“Viongozi wakuu wa chama, wabunge, wenyeviti wa mikoa, wilaya, majimbo na kanda kila mmoja atashiriki kwa nafasi yake katika operesheni hii. Tutafanya mikutano kwa wiki mbili, ila tunaweza kuongeza wiki nyingine moja.”Kwa habari zaidi Bofya na Endelea......

0 comments:
Post a Comment